Kikosi cha Maaskari 21 wa JWTZ waanza safari ya kupandisha mwenge wa Uhuru na Benderera ya Tanzania mlima Kilimanjaro

Kikosi cha Maaskari 21 wa Jeshi la Wananchi ( JWTZ) wameanza safari ya kupandisha mwenge wa Uhuru pamoja na Benderera ya Tanzania katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za Mwenge huo na ikiwa ni mara ya pili tangu kupandishwa Mwaka 1961.

Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) Miaka 60 ya Muungano pamoja na miaka 25 ya kifo cha Mhasisi wa Taifa hili Mwl Julias Kambarage Nyerere toka alipoaga Dunia.

Awali kabla ya kuanza safari hiyo ya kupandisha Mwenge huo wa Uhuru na Bendera ya Taifa kiongozi wa Msafara kutoka JWTZ Luteni Kanali Khalid Hamisi amesema watatekeleza jukumu walilopewa la kufikisha vitu vyote viwili katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana , Ajira, na watu wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete (Mb) ndiye Mgeni rasmi katika zoezi hilo la kupandisha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Zoezi hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar akiwemi Waziri wa Utalii Balozi Pindi Chana,Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana,Utamadauni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Fatuma Hamad   

Related Posts