MAOMBI 131 YA WAFUNGWA KUJADILIWA MWANZA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Jeremiah Yoram Katungu, jioni ya leo tarehe 16 Oktoba 2024, amempokea Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Balozi Khamis Kagasheki, pamoja na aliyekuwa Kamishna mstaafu wa Jeshi la Magereza, Juma Malewa. Ujumbe wa Bodi hiyo unatarajia kufanya kikao katika Mkoa wa Mwanza kujadili maombi ya wafungwa 131, ili kubaini wenye sifa za kunufaika na parole pamoja na wasiyo na sifa.

Parole ni mchakato wa kumruhusu mfungwa kutoka gerezani na kukamilisha kifungo chake akiwa uraiani, kwa masharti ya kuwa na tabia njema.

Kabla ya mapokezi hayo, CGP Jeremiah Yoram Katungu alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya matunda kadhaa katika eneo la Gereza Kuu Butimba.

Related Posts