Mrema akumbukwa Maonesho ya LANDROVER FESTIVAL .

Na Jane Edward, Arusha

Wadau wa sekta ya utalii kutoka kampuni ya Classic Tours&Safaris ambao ni wamiliki wa hotel ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo jijini Arusha wamesema uwepo wa maonyesho ya magari aina ya Landrover(LANDROVER FESTIVAL) imeleta fursa nyingi ya kuwakutanisha na watu kutoka maeneo mbalimbali na kupata fursa za kibiashara.

Beatrice Dimitris Dalaries ni meneja mkuu wa kampuni hiyo ambapo anasema kilele cha maonyesho hayo kama kampuni tanzu ya utalii wamepata nafasi ya kuonyesha magari yao ya landrover na wao wametumia siku hiyo katika kumuenzi muasisi wa kampuni hizo Maleu William Mrema.

Hata hivyo maonyesho hayo yanakadiriwa kuvunja rekodi kutokana na muitikio mkubwa wa washiriki kutoka nchi mbalimbali huku wajasiriamali wakipata fursa na kunufaika na maonyesho hayo.

 

Related Posts