Mwenezi CPA Makalla ajiandikisha kwenye daftari la wakaazi la wapiga kura

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Serikali za Mitaa TPDC Kata ya Mikocheni Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salam.leo tarehe 16 Octoba 2024.

Akizungumza na wakazi wa Mtaa wa TPDC Mikocheni mara baada ya kujiandikisha Mwenezi amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu sana na amefurahi kutimiza haki yake ya msingi ya kujiandikisha na amefurahishwa na jinsi watu wanavyojipanga na kuwa rahisi haichukui muda kisha akaendeelea kuwasihi watu ambao hawajiandikisha kwenda kujiandikisha kisha katika kipindi hiki kilichobaki.

Mwenezi ameongeza kuwa CCM inaridhika na muendelezo wa mchakato wa kujiandikisha na kuelekea siku za mwisho zilizobaki kutakuwa na hamasa kubwa ili watu wengi wajiandikishe kwenye daftari la Wapiga kura na hii inakuja bila kujali itikadi yeyote kwa ajili ya kuja kupata Viongozi wazuri wanataojali Wananchi.

Mwisho CPA Amos Makalla amesema unachokipanda ndicho unachokivuna wenzetu wameanza kulalamika tulitegemea haya mana hawakujipanga Sisi Viongozi wote kuanzia wa kitaifa mpaka ngazi ya chini tulienda kutoa hamasa ya kujiandikisha leo hii wenzetu wameanza kutafuta vijisababu watulie wafuate sheria sisi tumejipanga .

 

 

Related Posts