OnaStories Yaleta Mapinduzi katika Usafiri wa Daladala kwa Kutumia Teknolojia ya Uhalisia Pepe – MWANAHARAKATI MZALENDO

TAASISI ya OnaStories imezindua makala maalum kuhusiana na kada ya usafiri wa daladala kwa mfumo wa kidijitali, kwa lengo la kuifahamisha jamii ya Kitanzania na Kimataifa kutambua historia ya usafiri huo ulipoanzia.

Makala hii ni sehemu ya Mradi wa UTANZANIA, ambao unachunguza “Utanzania ni nini?” na kuuliza ni nini hasaa kinachomtambulisha Mtanzania halisi. Mradi huu unalenga kuwawezesha wabunifu wa Kitanzania kuandika na kuwasilisha hadithi zetu kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Akizungumza na waandishi hivi karibuni kwenye uzinduzi wa makala hiyo, Mkurugenzi wa Onastories, Princely Glorious amesema katika kipindi hiki mtu anawezaa kutazama makala kuhusu daladala, lakini wao wamekuja na kitu cha tofauti kwa kutengeneza maudhui ya uhalisia pepe (Virtual Reality) ambapo mtu akivaa miwani maalumu ya uhalisia pepe (Virtual Reality Headset) kilicho andaliwa naye anakuwa sehemu ya hiyo hadithi.

“Ukivaa hivi vifaa vinakuingiza na wewe kuwa sehemu ya hiyo hadithi sio tu mtazamaji bali muhusika kabisa” amesema Princely.

Kwa Upande wake,Msimuliaji wa Makala hiyo, Aurelio Mofuga amesema walihitaji kuonesha kuanzia usafiri ulipoanzia na sio matukio ya safari pekee ambayo yanahusisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (LATRA) amesema kupitia maudhui hayo yanaweza kuwasaidia katika kutanua uwanda wa matumizi ya Teknolojia ili kuwafikisha ujumbe watu.

OnaStories hujiusisha na kazi za maudhui ya hadithi katika uga wa usimulizi wa hadithi nchini Tanzania kupitia teklonojia kama vile uhalisia pepe (VR) na uhalisia ongezi (AR) na anuwai ya maudhui ya taswira.











Related Posts