Bodaboda Kigamboni kusafirisha bila malipo wenye mahitaji maalumu kujiandikisha

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

CHAMA Cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD), kimezindua huduma ya kuwasafirisha bila malipo watu wenye nahitaji maalumu kwenda na kurudi kujiandikisha katika Saftari la Mkazi wilayani Kigamboni.

Akizindua huduma hiyo, ,Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Pendo Mahalu,ameipongeza CMPD kwa hatua hiyo na kueleza itasadia klwatu wenye mahitaji maalumu kuandikishwa kwa wingi.

“ Hii mnayoifanya  CMPD ni kazi ya Mungu.Megusa kundi ambalo  nalo lina haki zake za msingi kushiriki uchaguzi, wazee, wenye ulemavu na watu wazima ,”amesema Pendo

Alieleza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, itambua mchango mkubwa wa CMPD hususan katika masuala ya kuinga mkono serikali chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan na kuahidi kuimarisha uhusiano huo.

Awali, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni,Erasto Kiwale, alisema watashirikiana kikamilifu na CMPD kuhakikisha walengwa wanatambuliwa na kufikiwa kupata huduma hiyo.

“Awali Mkuu wa Wilaya, alituelekeza kukutana na CMPD kuona namna wanaweza kutusaidia katika uhamasishaji. Tunashukuru kwa ubunifu huu mkubwa na ieleweke hii ni kazi ya kujitolea,”alieleza Kiwale.

Mwwnyekiti wa CMPD Wilaya ya Kigamboni, Patrick Kayanda, alieleza bodaboda na bajaji wilayani humo zitatoa huduma bila malipo ya kuwachukua majumbani watu wenye mahitaji maalumu na kiwapeleka katika vituo vya kujiandikisha.

“ Tutawarudisha majimbani bila malipo.Tayari hudumu imeanza kutolewa na tutaendelea hadi siku ya mwisho ya uandikishaji,”aliele Kayanda.

Alisema maofisa usafirishaji hao, wananafasi kubwa ya kutoa elimu ya uandikishaji kwani husafirisha wananchi wengi na kuzungumza nai kuhusu umuhimu wa kujiandikisha.

katibu wa CMPD  wilayani humo Kasabuku matias, alisema , kuns watu hawajui umuhimu wa kujiandikisha, wagonjwa, wenye ulemavu na wazee watahudumiwa,” alibainisha.

Alisema CMPD iliona  ni vyena makundi hayo yakasaidiwa kupata haki ya kujiandikisha na kupata fursa ya kupiga kura muchagua viongozi wanao wataka.

Alisema lengo lingine ni kuiunga mkono serikali chini ya Rais Dk. Samia kuhakikisha  wananchi wengi wana jiandikisha.

Zoezi la uandikishaji wananchi katika Daftari la Mkazi lilizinduliwa ba Rais Dk. Samia, Oktoba 11 mwaka huu na linatarajia kumalizika Oktoba 20 mwaka huu ambapo uchaguzi wa Serikali za Mitaa umeoangwa kufanyika Novemba27 mwaka huu.

Related Posts