Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imezindua kampeni maalum inayowalenga wateja wa migahawa ya KFC jijini Dar es Salaam, ambapo wanapata fursa ya kushiriki Tamasha la Chakula la Coca-Cola linalotarajiwa kufanyika Novemba sambamba na zawadi kemkem kutoka Coca-Cola.
Kampeni hii, iitwayo ‘Food Pass’, inatoa zawadi mablimbali kwa wateja watakaonunua chakula maalum cha “Pamoja-Coke Fest Meal”, ambacho kinajumuisha vipande vinne vya kuku, chipsi, na Coca-Cola.
Wateja watakaonunua chakula hicho katika vituo vya KFC ikiwemo Mlimani City, Mikocheni Plaza, Mbezi Beach, Magomeni, Diamond Plaza, na Kariakoo wataweza kujisajili kwa ajili ya kupata kijitabu cha ‘Food Pass’. Kijitabu hiki kitawapa fursa ya kuingia bure kwenye tamasha la kufunga Coca-Cola Food Fest litakalofanyika mwezi Novemba.
Kila mteja anapopata chakula hiki, kijitabu chake cha ‘Food Pass’ kitapigwa muhuri, na mihuri hiyo itafungua zawadi mbalimbali, huku wateja 1,000 wa kwanza wakipata tiketi za bure za kuingia kwenye tamasha. Kampeni hii itafanyika kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 22.
Kabula Nshimo, Meneja wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania, alisema kuwa kampeni hii ni sehemu ya muendelezo wa Coca-Cola Food Fest inayoadhimisha vyakula mbalimbali na bidhaa za Coca-Cola kote nchini.
Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Masoko-Coca-Cola Tanzania (kulia) na Shafii Abbas Idege, Meneja wa Operesheni-KFC Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Food Pass inayowalenga wateja wa migahawa ya KFC jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa Kampeni hiyo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kampeni ya Food Pass inawapa wateja fursa ya kujipatia zawadi mbalimbali kutoka Coca-Cola sambamba na tiketi ya bure ya kushiriki katika Tamasha kubwa la Chakula la Coca-Cola linalotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.