DKT. BITEKO NA WAZIRI WA NYUMBA MISRI KUSIMAMIA UKAMILISHAJI MRADI WA JNHPP

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 17, 2024 jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nyumba, Huduma na Jumuiya za Mijini kutoka nchini Misri, Mhe. Sherif EI Sherbiny.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kusimamia wakandarasi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kukamilisha mradi huo kwa wakati ambao hadi sasa umefikia asilimia 99 ya utekelezaji wake.

Aidha, Mhe. EI Sherbiny ambaye ameteuliwa hivi karibuni katika nafasi hiyo akiwa nchini atataembelea mradi wa JNHPP.

Related Posts