KAWAIDA NA KISIPIKA KUHAMASISHA UANDIKISHAJI BIHARAMULO SOKONI

Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Ndg. Mohammed Ali Kawaida ameongoza zoezi la kuhamasisha wananchi wa wilaya ya Biharamulo kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la makaazi.

Ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara yake mkoani Kagera Ndg. Kawaida ameendelea na ziara yake leoOktoba 17, mwaka huu wilayani Biharamulo ambapo ameamua kutembea kwa mguu kwenye soko la Biharamulo mjini na kuwahamasisha wananchi ambao walikuwa sokoni hapo wakifanya shughuli zao za uchuuzi ikiwa ni siku ya gulio na kuwaeleza umuhimu wa kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, mwaka huu.

Hata hivyo @comrade_kawaida amewapongeza wananchi wote wa Biharamulo wakiongozwa na mbunge wao Mhe. @ezra_chiwelesa ambao tayari wameshatumia haki yao ya msingi kujiandikisha huku akiwasihi waendelee kuwahamasisha wale waliobaki kuendelea kushiriki zoezi hilo kwa kuwa siku zimebaki chache.

Aidha Mwenyekiti Kawaida akiwa mjini Biharamulo amepata fursa ya kuongea na maafisa usafirishaji katika standi kuu ya mabasi ya Biharamulo akiwahamasisha kuendelea kujiandikisha zikiwa zimebaki siku tatu ili zoezi hilo lifungwe

Related Posts