Makamba apiga kambi Bumbuli,kuongeza kasi ya uandikishaji.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba amewataka wakazi wa jimbo hilo kuendeleza kasi ya kujiandikisha ili kufikia au kupita lengo lilojiwekea la uandikishaji.

Mbunge huyo ambaye amepiga kambi jimboni kwa ajili ya kuhamasisha uandikishaji amewapongeza wakazi wa jimbo hilo kwa kujitokeza kwa wingi na kuwezesha halmashauri ya Bumbuli kuwa miongoni mwa halmashauri zinazofanya vizuri kati ya halmahauri zote 11 za mkoa wa Tanga katika zoezi la uandikishaji lilloanza Oktoba 10.

Takwimu zinaonyesha kua hadi kufikia tarehe 16 wapiga kura 68,828 wamekwisha andikishwa ikiwa ni asilimia 76.7 ya lengo.

Aliwataka wakazi hao wa Bumbuli kuongeza kasi na kusisitiza kuwa ili Chama Cha Mapinduzi (CCM) kishinde kwa kishindo lazima wanachama na washabiki wa chama hicho pamoja na wananchi wote wajiandikishe na kukipigia kura kipate ushindi mkubwa.

Kwa mujibu wa takwimu zilozotolewa na Waziri wa Nchi katiika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa mkoa wa Tanga hadi kufikia Oktoba 14 ulikuwa miongoni mwa mikoa iliyokuwa inaongoza kwa uandikishaji ukiwa una asilimia 54 hadi kufikia tarehe hiyo.

Makamba alisema kuwa kwa kasi hiyo halmashauri hiyo ina uwezo wa kufikia lengo ililojiwekea la uandikishaji ifikapo tarehe ya mwisho.

Mbunge huyo alisema kuwa CCM katika Halmashari ya Bumbuli imejipanga kushinda kwa kishindo vijiji na vitongoji vyote katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mkurugenzi Halmashauri hiyo, Baraka Zikatimu, Jimbo la Bumbuli limepanga kuandikisha wapiga kura 88,395 ambapo kati ya hao wanawake ni 43,644 na wanaume wakiwa 42,751.


Related Posts