TASAC YASHIRIKI MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA LOJISTIKI NA UCHUKUZI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Lojistiki na Uchukuzi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo tarehe 17 Oktoba, 2024.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi amesema Serikali inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 600 kwa ajili ya kugharamia miradi mitatu itakayoboresha huduma ya usafirishaji kwa njia ya maji mkoani Kigoma na maeneo yanayozunguka.

Mhe. Prof. Mbarawa amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha meli, ujenzi wa meli ya mizigo pamoja na meli ya kisasa ya abiria inayotarajiwa kufanya safari zake katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria.

“Bandari ya Kigoma ni muhimu kwa sababu kwenye Ziwa Tanganyika tunapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kule kuna madini, kutokana na hilo kama Serikali tumeona tuweke
 

Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Salum Mohamed akizungumza katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Lojistiki na Uchukuzi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo tarehe 17 Oktoba, 2024
Mkurugenzi  Mkuu wa TASAC  Salum Mohemed watatu kutoka kushoto akiwa katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Lojistiki na Uchukuzi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo tarehe 17 Oktoba, 2024
 

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  Mkuu wa TASAC Salum Mohamed wakati alipotembelea banda la TASAC katika maonesho kwenye  Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Lojistiki na Uchukuzi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam leo tarehe 17 Oktoba, 2024

Related Posts