Alhamisi Kilombero, Morogoro 17 October 2024 Wakulima wa miwa Bonge la Kilombero wameombwa kutumia elimu kutatua changamoto zinazowakabili kwenye kilimo chao cha miwa.
Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof Kenneth Bengesi wakati akifunga maonyesho ya siku tatu ya wakulima wa miwa Bonde la Kilombero pamoja na wadau wa kilimo ambayo yalifanyika Kilombero.
‘Naomba niwapongeze wakulima wa miwa wa Bonde la Kilombero kwa kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho ya mwaka. Kujitokeza kwenye ndio kumefanya maonyesha haya kuwa ya kipekee kwa mwaka huu’, alisema Pro Bengesi.
Pro Bengesi aliongeza, ‘Kwenye maonyesha hayo, nina uhakika mmekutana na wataalum wengi ambao wamewapa elimu na mbinu za kuongeza uzalishaji. Nawaomba mkatumie elimu hiyo kwenye kutatua changamoto ambazo mnakutana nazo kwenye kilimo cha miwa ili muweze kuongeza uzalishaji’.
Siku ya Wakulima wa Miwa Kilombero ilianza na mdahalo ambapo wakulima wa miwa Bonde la Kilombero walipata fursa ya kutoa changamoto zao mbele ya wataalum wa kilimo hicho na kufuatiwa na maonesho ya siku tatu ambayo yalijumuisha vifaa mbalimbali vya kilimo, mbegu bora, matumizi sahihi ya mbolea, na mbinu mbalimbali za kudhibiti magonjwa na wadudu katika zao la miwa
002
Mwenyekiti wa Maonesho ya Siku ya Wakulima wa Miwa Kilombero Victor Byemelwa ambaye pia ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Wadau Kilombero Sugar akipokea cheti kutoka na utendaji wake kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof Kenneth Bengesi wakati wa kufungua Siku ya Wakulima wa Miwa Bonde la Kilombero pamoja na maonyesho ya siku tatu ambayo yalijumuisha vifaa mbalimbali vya kilimo, mbegu bora, matumizi sahihi ya mbolea, na mbinu mbalimbali za kudhibiti magonjwa na wadudu katika zao la miwa
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Kibaha John Msemwa akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof Kenneth Bengesi kutembelea mashamba ya miwa ya Kilombero wakati wa kufunga Siku ya Wakulima wa Miwa Bonde la Kilombero pamoja na maonyesho ya siku tatu ambayo yalijumuisha vifaa mbalimbali vya kilimo, mbegu bora, matumizi sahihi ya mbolea, na mbinu mbalimbali za kudhibiti magonjwa na wadudu katika zao la miwa.
Ends.