Baada ya kupokelewa na Rais Steinmeier, mapokezi ambayo yaliambatana na kwa gwaride la kijeshi Biden alitunukiwa tuzo ya juu zaidi ya Ujerumani, ijulikano kama “Grand Cross of the Order of Merit” mjini Berlin. Kwa kupokea tuzo hiyo, kiongozi huyo sasa anakuwa wa pili baada ya George H. W. Bush.
Katika kauli yake ya mwanzo katika ziara yake hiyo Biden amesema ni lazima wadumishe msaada wao kwa Ukraine, amemlaani Rais Putini kwa mashambilizi yake dhidi ya Ukraine na kusema NATO bado ipo madhubuti na pamoja kuliko huko nyuma.
Majadiliano kuhusu Urusi na Ukraine na Mashariki ya Kati
Lakini baadae kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81, atafanya mazungumzo yenye kuhusisha masuala ya mataifa mawili, lake na Ujerumani na Kansela, Olaf Scholz, ikiwa ni kabla ya mkutano wake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.
Mazungumzo hayo huenda yakalenga zaidi vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, ambayo yote yamekuwa na mabadiliko makubwa sana katika siku za hivi karibuni. Biden amewasili mji Berlin katika kipindi kifupi baada tangazo la Israel kwamba shambulizi lake limemuua kiongozi wa Hamas Yehya al-Sinwar, hatua wanayoitazama kama itatoa kutoa fursa ya kumalizika kwa mzozo wa mwaka mzima huko Gaza na kuachiwa huru mateka wa Israel waliosalia.
Soma zaidi:Biden kukutana na viongozi wa Ulaya Ijumaa
Kansela Scholz na Biden pia wanatarajiwa kumjadili Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kile mwenye anachokiita “mpango wa ushindi” uliosubiriwa kwa muda mrefu, ambao aliutangaza juma hili katika kipindi ambacho pia kimegubikwa na hatua za kusonga mbele kijeshi za Urusi huko mashariki mwa Ukraine.
Katika pendekezo lake Rais Zelensky kuna hitaji la Ukraine kujumishwa haraka katika kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, pamoja na maombi ya ruhusa ya kutumia silaha za masafa marefu za Magharibi dhidi ya kuyalenga maeneo ya ndani zaidi katika ardhi ya Urusi, kwa lengo ya kuilazimisha serikali ya Moscow kufanya mazungumzo ya kumaliza vita.
Wasiwasi wa Ujerumani na Marekani katika mapambano dhidi ya Urusi
Mataifa ya Marekani na Ujerumani yamekuwa muhimu zaidi kwa Ukraine katika utoaji wa misaada ya kijeshi na kifedha, lakini Kansela Scholz na Rais Biden walipinga matakwa ya hivi karibuni ya Zelensky, wakihofia kuingizwa katika mapambano ya moja kwa moja na Urusi.
Ikumbukwe tu kwamba safari hii ya Bideninafanyika ikiwa ni takribani zaidi ya juma baada ya kughairi mipango yake ya awali ya kufanya safari ya hadi Ujerumani kutokana na Kimbunga Milton.
Chanzo DPA