RIPOTI YA ESG YABAINI CHANGAMOTO KATIKA MAZINGIRA YA JAMII NA UTAWALA

 Mtendaji Mkuu wa Chama wa Waajiri Tanzania (ATE) wa pili kulia, Laura Gren, Afisa Programu Mwandamizi wa shughuli za kazi za waajiri kutoka shirika la kazi duniani (ILO), wa kwanza kulia, Jane Sorogo Afisa kazi Mkuu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa kwanza kushoto na Mkurugenzi wa Afya, usalama na mazingira Kazini kutoka Tukta (wa pili kushoti) wakionyesha ripoti ya Environment Social Governance (ESG) iliyozinduliwa leo Oktoba 18,2024 na ATE kwa kushirikiana na ILO kuangalia jinsi gani masuala ya mazingira ya kijamii, uongozi na makampuni yanazingatiwa.

Mtendaji Mkuu wa Chama wa Waajiri Tanzania (ATE) Suzzane Ndomba- Doran akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Environment Social Governance (ESG) iliyozinduliwa leo Oktoba 18,2024 na ATE kwa kushirikiana na ILO kuangalia jinsi gani masuala ya mazingira ya kijamii, uongozi na makampuni yanazingatiwa.

Laura Green, Afisa Programu Mwandamizi wa shughuli za kazi za waajiri kutoka shirika la kazi duniani (ILO), akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Environment Social Governance (ESG) leo Oktoba 18,2024 ǰijiniDaresSalaam. Ripoti imelenga kuangalia jinsi gani masuala ya mazingira ya kijamii, uongozi na makampuni yanazingatiwa.

RIPOTI ya utafiti uliyochunguza mazingira ya Jamii na Utawala (ESG) nchini Tanzania imebaini changamoto nane kuu, ambapo kizuizi kikubwa ni mtazamo ulioenea kuhusu maendeleo endelevu.

Ripoti hiyo iliyopewa jina ‘Hali ya ESG nchini Tanzania’ uliofanywa na Shirikisho la Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushiikiana na shirika la Kazi Duniani (ILO) umeonyesha umuhimu wa mabadiliko ya kitamaduni katika biashara na kushughulikia ukosefu wa uelewa wa pamoja na tofauti za sekta.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran, ameyasema hayo leo Oktoba 18, 2024, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa utafiti huo, akionyesha kuwa lengo la utafiti ni kusaidia biashara kukabiliana na mabadiliko ya matarajio na viwango katika mazoea ya jamii na serikali.

Amesema ripoti hiyo iliyofanywa katika sekta kumi muhimu ikiwa ni pamoja na kilimo, sekta yamadini, fedha/banking, utalii, na viwanda.

Akitaja baadhi ya changamoto kuu ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo na wa vipande, kukosekana kwa uelewa wa pamoja wa ESG kati ya kampuni za Tanzania, hali inayosababisha viwango tofauti vya uelewa na ufahamu na tofauti kati ya kampuni za ndani na za kimataifa.

Changamoto nyingine ni kampuni za kimataifa zinaonyesha utekelezaji mkubwa wa mazoea ya ESG, huku kampuni za ndani zikiwa nyuma. Kampuni kubwa huwa zinakumbatia ESG zaidi ikilinganishwa na ndogo na athari za sekta maalum.

Ndomba-Doran amesisitiza umuhimu wa mabadiliko ya kitamaduni kuelekea maendeleo uendelevu, ambapo ESG inatakiwa kuangaliwa si tu kama suala la kufuata sheria, bali kama kipengele muhimu katika biashara.

Ameonyesha kuwa kuna haja ya mbinu mbili za kuimarisha mazoea ya ESG nchini Tanzania, kuimarisha mifumo ya kanuni ili kuhakikisha kufuata viwango vya ESG na kubadilisha mtazamo.

Ndomba-Doran amesisitiza kuwa kanuni za ESG zinakuwa muhimu zaidi kwani zinavyoathiri mazoea ya kampuni yanayohusiana na uendelevu wa mazingira, uwajibikaji wa kijamii, na utawala wa kampuni.

Ameongeza kuwa kwa kutumia utafiti wa pande tatu kuhusu ESG, ATE inaweza kusaidia katika kufanya maamuzi, kutetea mazoea ya ESG kupitia mpango wa pande tatu, na kutoa huduma za kisheria kusaidia biashara kufikia ufautaji wa ESG.

Kwa Upande wa Jamal Baruti kutoka Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) amesema kuwa utafiti huo unaonesha namna bora ya uhifadhi wa mazingira na kuhakikisha biashara zinakuwa na maendeleo endelevvu.

“Tunaelekea katika mabadiliko ya hiari ya mtazamo ambayo inatazamia kuingiza mazingira ya Jamii na Utawala katika mtaala wa elimu, kuhamasisha, na kutumia mifano mizuri ya mazoea kuonyesha ESG kama kichocheo cha biashara.”

Tukio hilo lilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), watengenezaji, mashirika ya kijamii na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Related Posts