Kilimanjaro Premium Lager International Marathon yazinduliwa rasmi Dar

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana ( wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Khensani Mkhombo (wa tatu kushoto) wakiongoza wageni wengine katika uzinduzi rasmi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025 Jijini Dar es Salaam Ijumaa. Wengine kutoka kushoto ni mwakilishi wa Chama Cha Riadha Tanzania, Felix Chunga, Meneja Chapa wa Kampuni ya Tigo Woinde Shisael, Afisa Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania Charles Maguzu na Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Henry Tandau.

 Meneja Chapa wa Kampuni ya Tigo, Woinde Shisael.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Khensani Mkhombo.

MBIO za Kimataifa za Masafa Marefu za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon zimezinduliwa rasmi  kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kuanza kwa mbio hizo ifikapo Februari 23, 2025.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana alitangaza kuwa wizara yake ipo tayari kukaa pamoja na waandaaji wa tukio hili muhimu na kuona njia ambazo zinaweza kukuza utalii wa ndani na wa kimataifa.

Alisema mbio za masafa marefu zimeonekana kuwa ni moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo nchini, hivyo ni jukwaa zuri la kukuza utalii. 

“Tunajivunia mbio za masafa marefu za Kilimanjaro Premium Lager kwani zimeonekana kuwa miongoni mwa matukio makubwa ya kimataifa katika kanda kwani zinawaleta pamoja zaidi ya washiriki 12,000 na idadi sawa ya watazamaji kutoka zaidi ya nchi 56 na wote hawa ni watalii watarajiwa. Hii ni hatua kubwa sana,” alisema Dk Chana.

 Alieleza kwamba wizara kabla na baada ya tukio hilo, itatangaza vivutio vya utalii vya kutosha kupitia tukio hili kubwa ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanafikiwa kadiri iwezekanavyo.

Alibainisha zaidi kwamba mbio za kimataifa za masafa marefu za Kilimanjaro Premium Lager zinazohusisha mboo za Km 42, km21 na  km 5, zimeongeza mchango mkubwa kwa utalii wa michezo na hii imeisaidia sana serikali katika kutekeleza sera za utalii na michezo.

“Nawapongeza wadhamini wote wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager (mdhamini mkuu) na Tigo (kilomita 21), Wadhamini wa mezani za maji ni Simba Cement, CRDB Bank, Kilimanjaro Water, TotalEnergies na TPC Sugar. Wasambazaji rasmi ni GardaWorld Security, CMC Automobiles, Sal Salinero Hotel na watoa huduma maalumu – Kibo Palace Hotel na Hoteli ya Keys. Bila nyinyi isingekuwa rahisi,” alisisitiza.

Waziri pia aliwataka washiriki na watazamaji kutumia msimu wa mbio za masafa marefu kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii, ikiwa ni pamoja na Mlima Kilimanjaro, Serengeti, Ngorongoro, Zanzibar na vivutio vingine.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited Khensani Mkhombo alisema wanajivunia kupitia Kilimanjaro Premium Lager, kudhamini tukio hilo kwa miaka 23 iliyopita, na kuufanya kuwa moja ya udhamini mrefu zaidi

nchini Tanzania na kuongeza kwamba miaka yote hii wametiwa moyo na msaada wa utalii na

utamaduni wa Watanzania kwa jumla – ambao tukio hili linasaidia kuukuza.

Alitoa wito kwa washiriki kujiandikisha kwa wakati kwani usajili tayari umeshafunguliwa mtandaoni kupitia www.kilimanjaromarathon.com na kupitia TigoPesa.

Kwa mara nyingine tena aliahidi kwamba itakuwa wikendi ya shughuli za kufurahisha kuhusu mbio za masafa marefu na hivyo washiriki wanapaswa kupanga kukaa kwa muda mrefu Moshi na kufurahia ukarimu wa Kilimanjaro Premium Lager na yote yatakayofanyika ndani na karibu na mji na kisha siku ya tukio lenyewe pia.

Meneja Chapa wa Kampuni ya Tigo, Woinde Shisael alisema kwa vile Tigo inaadhimisha miaka 30 ya kubadilisha maisha kupitia ubunifu wa kidijitali na kuadhimisha miaka 10 ya kujivunia kudhamini Tigo Kili Nusu Marathoni, kujitolea kwa uwekezaji wa mtandao huhakikisha kwamba washiriki na watazamaji wanaweza kufurahia muda wote tukio hili muhimu.

Zaidi ya michezo, alisema, ubia wa sasa unaonyesha kujitolea kwao kukuza vipaji, mtindo wa maisha bora, na kusaidia jamii nchini Tanzania. “Tunatazamia mbio za kusisimua na muongo mwingine wa kuwawezesha Watanzania kupitia michezo na teknolojia,” aliongeza.

Alisema kwamba jukwaa lao la ubunifu na lililorahisishwa la usajili na malipo ya mbio za masafa marefu liko wazi kwa makundi yote yatakayoshiriki. 

Mkiambiaji anaweza kupiga *150*01#, kisha kubonyeza 5 LKS, halafu kubonyeza 5 (tiketi) na kufuata maelekezo ya kukamilisha usajili.

Jukwaa hili la malipo limeleta mapinduzi makubwa namna wakimbiaji Watanzania wanavyoweza kujisajili chaguo rahisi kuingia. Timu ya Tigo imefanya kazi bila kuchoka na timu ya Usimamizi wa Mbio za Kimataifa za Masafa Marefu ili kuweka chaguo hili la malipo kama mpango wa kuongeza thamani kwa soko la ndani.

Mwaka huu mbio za burudani za kilomita 5 na zinazoungwa mkono vyema ambazo washiriki wake huwa familia na watu wapya wanaokuja barabarani.

 

Waandaaji wa tukio hili walitoa wito kwa wakimbiaji kutumia fursa ya ada ya kiingilio cha awali kuanzia Oktoba 21 hadi usiku wa manane wa Disemba 12, ambapo baada ya hapo ada za kuingia zitaongezeka kwa makundi na kwa mataifa yote kuanzia Disemba 13 hadi usiku wa manane wa Februari 3, 2025 au hadi ziishe – chochote kitakachokuwa cha mapema kwa vile kuna nafasi chache. 

Utaratibu wa huduma ni kwamba wanaofika mapema ndio watakaohudumiwa kwanza. 

Waandalizi wangependa pia kuwashukuru wadhamini wao wakuu Kilimanjaro Premium Lager na Tigo kwa kutenga jumla ya shilingi milioni 53.5, ikiwa ni zawadi za mbio za masafa marefu na nusu mbio na zawadi za makundi mbalimbali.

Waandaji pia walisema kwamba tukio hili mwaka ujao pia litasaidi Shirika la Hisani la Tumaini la Maisha (TLM), ambalo linalenga kumfikia kila mtoto nchini Tanzania aliye na saratani, na kumtibu kwa ubora wa hali ya juu bila malipo (bure) kwa matumaini ya kuendelea na afya bora na kuongeza asilimia 5 ya fedha kutoka kwa kila kiingilio kitakacholipwa zitakwenda kwa shirika la hisani.

Tena fedha zote zitakazochangwa kwa TLM kwenye tukio la 2025 zitaelekezwa kwenye Hospitali ya KCMC iliyopo mjini Moshi, kusaidia Wodi ya Watoto wa Saratani. “KCMC ni mbia muhimu wa mbio za masafa marefu kutokana na msaada wake wa matibabu kwenye tukio na eneo la kumalizia kila mwaka na imekuwa msaada kwa wakimbiaji wanapopita karibu na hospitali hii siku ya mbio hizo,” alisema mmoja wa waandaaji.

Mbio za Kimataifa za Masafa Marefu za Kilimanjaro Premium Lager zitakazofanyika Jumapili Februari 23, 2025 kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), zimeandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na nchini Tanzania zinaratibiwa na Executive Solutions Limited. Wild Frontiers Events inawajibika kwa shughuli zote za safari za ndani na utangazaji wa kimataifa wa tukio hilo.

Related Posts