Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiajiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika mtaa wa Ndemanilwa kata ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi tarehe 19 Oktoba 2024.
**********************
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geophrey Pinda ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mhe. Pinda amejiandikisha leo jumamosi katika mtaa wa Ndemanilwa katika kata ya kibaoni halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Kwa mujibu wa mwandikishaji wa kituo hicho Bw. Dikson Fabian zoezi la uandikishaji katika kituo chake limeenda vizuri na kwa mafanikio makubwa ambapo takriban watu 1,090 wamejitokeza.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbe Mhe. Geophrey Pinda amesema, kwa kumbukumbu za jimbo lake zinaonesha watu wengi wamejitokeza kujiandikisha.
‘’Nitoe wito kwa watu wote ambao hawajajitokeza kujiandikisha wajitikeze kwa ajili ya kushiriki kuchagua viongozi ambao ni uhitaji wao’’ alisema Mhe. Pinda.