WAAJIRI HEALTH BONANZA LAFANA, WAKUMBUSHWA KUPIMA AFYA MARA KWA MARA

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Jakaya Kikwete amewakumbusha waajiri na Wafanyakazi kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara ili kupunguza athari zinazotokana na magonjwa ya kuambukiza kama kisukari na shinikizo la damu.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 19,2024 wakati wa Waajiri Health Bonanza lililofanyika katika viwanja vya mchezo vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam lililokuwa na kaulimbiu ya “Zuia magonjwa yasiyoambukiza, ongeza ufanisi kazini”. Amesema kuwa Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambikizwa yanahitaji nguvu ya pamoja ili kuyatokomeza.

“Kwa kuzingatia hilo serikali kwa kushirikiana na wadau inafanya kampeni na maadhimisho ya kitaifa kwaajili ya kuhamasisha jamii kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara. In”

“Takwimu zinaonesha wenye umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wanashinikizo la juu la damu, kisukari na uzito uliozidi ingawa serikali ndio inategemea nguvu kazi hiyo.” Ameeleza Ridhiwani Kikwete

Pia amewasisitiza waajiri wote kuzingatia sheria ya usalama wa afya mahala pa kazi na kujenga mazingira wezeshi kwa watu wote hususani watu wenye ulemavu ili kuwa na uchumi shirikishi na wa ushindani.

Licha ya hayo Waziri Kikwete amewapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kuandaa ‘Waajiri Health Bonanza’ ili kuwaweka pamoja katika michezo mbalimbali.

Pia amezindua Mwongozo wa VVU na Ukimwi na magonjwa yasiyoambukizwa ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,

Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu unaopaswa kutumiwa na waajiri hususani katika sekta binafsi.

Akiwasilisha salamu zake kutoka ILO, Mkurugezi wa shirika la kazi duniani (ILO) katika ukanda wa Afrika Mashariki, Caroline Lugala amewapongeza ATE kwa kuongoza vyema sekta binafsi pia kwa kuendeleza bonanza la Waajiri Afya la 2024.

“Kuandaliwa kwa bonanza la tatu la Waajiri la Afya 2024 ni uthibitisho tosha wa uwezo wa ATE kusimamia, kuendeleza na kuboresha ufanisi, uratibu na uwakilishi wa wapamoja wa sekta binafsi, ushirikiano wa afya na uzuiaji wa VVU hasa mahala pa kazi na kwenye jamii kwa ujumla” Ameeleza

Pia ametoa wito kwa wadau wote wa maendeleo, sekta binafsi na sekta ya uuma katika mpango wa kuendeleza bonanza hilo la Afya.

Ameeleza kuwa ILO kwa kushirikiana na wadau wake wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzuia magonjwa yasiyoambukiza na kuboresha tija mahala pa kazi kwa kufanya utafiti, kukusanya taarifa za athari za magonjwa yasioambukiza kwenye jamii na ili kuwezesha sera za kukuza usalama mahala pa kazi.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran amewashukuru waajiri na wafanyakazi waliojitokea katika bonaza la waajiri la Afya katika viwanja vya UDSM jijini Dar es Salaam.

Bonanza hilo limeandaliwa na ATE kwa kushirikiana na shirika la Kazi duniani (ILO),OSHA, WCF, NSSSF, Helios Towers, Smiles, Dental Clinic na Shifaa hospital na kufadhiliwa na Benki ya NMB, Alaf Tanzania, DP Wold, Swissport, mcc,Stanbic bank, Cool Blue G4S na SGA.

Matukio mbalimbali katika bonanza la Waajiri la Afya katika bonanza liliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Oktoba 19, 2024.

Related Posts