Alikiba atunukiwa TUZO kama CHAMPION wa Maendeleo ya Mtoto wa Kike

Alikiba atunukiwa TUZO kama CHAMPION wa Maendeleo ya Mtoto wa Kike kupitia Kongamano la KIGODA LA WASICHANA @kigodachawasichana lililofanyika Tarehe 11/10/2024 katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Kike visiwani Zanzibar. Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya @shirazfoundation imemkabidhi Tuzo hiyo Alikiba alipohudhuria na kushiriki Kongamano hilo viwanja vya Nyamanzi Zanzibar na kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (SMZ) Riziki Pembe, Mgeni Maalum na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zena Said @zenasaidzas na Mgeni Maalum na Mlezi wa Jukwaa hilo Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Bi Mgeni Juma.

Alikiba alipongeza Jukwaa hilo la KIGODA CHA WASICHANA na kuahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika mambo mengine ya Kijamii na kuendelea kumuwezesha Mtoto wa Kike.

 

#GirlChildDay #Zanzibar

Related Posts