ZOEZI LA UANDIKISHAJI LATAMATIKA KWA AMANI

Na Linda Akyoo -Moshi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdun Babu ameeleza namna alivyo furahishwa na zoezi la uandikishaji Wilaya ya Same linavyotamatika kwa amani na utulivu, huku akiipongeza kamati ya usalama ya Wilaya kwa kazi nzuri ya kuimarisha usalama ndani ya siku zote 10 za uandikishaji kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu wa 2024.

RC Babu amezungumza hayo akiwa Wilaya ya Same kwenye ziara yake ya kukagua hali ya zoezi la Uandikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi, ambapo amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Novemba 27, 2024 kuchagua viongozi wao wa Vijiji,Vitongoji na Mitaa wanaowataka ikiwa ni haki yao kikatiba.

Aidha Mhe.Babu amesema zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 Mkoani Kilimanjaro litafanyika kwa uwazi pamoja na amani kuhakikisha wananchi wote wanashiriki kuchagua viongozi wao.



Related Posts