🥊 ZULFA MACHO NA SAIDI KANENDA KUPANDA ULINGONI LEO ROBO FAINALI UBINGWA WA AFRIKA AFBC

▫️Zulfa dhidi ya Bisambu Merveille mwenyeji wa DR Congo

▫️Kanenda dhidi ya Amroug El Abidine kutoka Morocco 

 

21-10-2024, Kinshasa – DR Congo: Mabondia wa Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi “Faru Weusi” Zulfa Macho na Saidi Hamisi Kanenda wanatarijiwa kupanda ulingoni leo katika mashindano ya AFBC Ubingwa wa Afrika – Kinshasa 2024 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

Zulfa atapanda ulingoni katika session ya 4 majira ya alasiri (muda wa Kinshasa Gmt +1) dhidi ya mpinzani wake Bisambu Merveille, mwenyeji wa DR Congo katika uzani wa Bantamweight 54kg.

 

Saidi Kanenda naye atapanda ulingoni usiku wa leo katika session ya 5 uzani wa Light middleweight 71kg dhidi ya Amroug El Abidine kutoka Morocco. 

 

Mashindano haya yameanza rasmi tarehe 18-10-2024 na yatafikia tamati kwa fainali kuchezwa siku ya Jumamosi 26-10-2024.

 

Tanzania inawakilishwa na mabondia watatu (3) ambao ni Saidi Kanenda (Light middleweight 71kg), Zulfa Macho (Bantam 54kg) na Najma Isike (Light welterweight 63kg) huku wakisimamiwa na Mwalimu Mkuu IBA 1 Star Samwel Kapungu.

 

“Mungu wabariki Zulfa na Kanenda, Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿”

 

✍🏽 Ofisi ya Rais – BFT 

 

Related Posts