BILIONI 13.5 KUJENGA JENGO LA TAALUMA TIA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima O. Dengego ameipongeza TIA kwa andiko zuri lililoipelekea Serikali ya awamu ya sita kupitia mradi wa HEET kuipatia Bilioni 13.5 kujenga jengo la kisasa la Taaluma Kampasi ya Singida,

“Mkoa wa Singida unaenda kuwa jiji, hivyo ni lazima na taasisi zetu ziwe na muonekano wa jiji, ujenzi wa jengo hili lazima uwe wa kisasa na wa kiwango cha juu, mkandarasi tutakuwa sambamba ili thamani ya pesa ionekane,”. Alisema Mhe. RC

Mhe. Halima amesema hayo wakati wa halfa fupi ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa mradi huo baina ya TIA na mkandarasi SALEM Constructor”, iliyofanyika ukumbi wa Msonge, Kampasi ya Singida.

Afisa Mtendaji Mkuu Profesa William Pallangyo, amesema TIA Kampasi ya Singida itaenda kubadilika kwa ujenzi wa kisasa wa jengo lenye ghorofa tatu ambao utachukua takribani miaka miezi 24 hadi kukamilika kwake, na utaenda kuhudumia watu 3,637,

“Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizi za mradi wa HEET, ambapo zinaenda kuboresha mazingira ya kujisomea na kufundishia,”. Alisema Profesa Pallangyo

Profesa Pallangyo amesema amepokea maelekezo ya Mhe. Mkuu wa mkoa wa Singida ya kuhakikisha mkandarasi anajenga kwa kuzingatia makubiliano ya mkataba, kwa wakati na kwa viwango vya juu na kisasa.

Naye, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SALEM “Constructor” Charles Kasmir amesema watahakikisha wanazingitia mkataba wa makubaliano, maelekezo yalitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kujenga jengo la kisasa, lenye viwango litakaloonesha thamani ya pesa, na kukamilika kwa wakati ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania.


 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dengego akihutubia Wananchi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya eneo la mradi baina ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania na mkandarasi SALEM Constructor
 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William Pallangyo akiongea na Wananchi katika Halfa fupi ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa mradi wa Kampasi ya Singida na mkandarasi SALEM Constructor

Related Posts