MSAJILI WA HAZINA MCHECHU AIPONGEZA NELSONA MANDELA KWA TAFITI NA BUNIFU ZINAZOTATUA CHANGAMOTO 

 

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Henry Kahimba (Kushoto) alipotembelea Maabara ya Taasisi hiyo.

Na Mwandishi Wetu

 

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu aipongezi Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kufanya vizuri katika tafiti na bunifu mbalimbali zinazotatua changamoto za jamii na kuchangia katika uchumi wa viwanda.

Akizungumza na menejimenti ya taasisi hiyo katika ziara yake Oktoba 21, 2024 Tengeru jijini Arusha ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo inapaswa kuangaliwa kwa jicho la umuhimu ili kuongeza uzalishaji wa bunifu mbalimbali kupitia tafiti zinazofanyika.

“Taasisi hii ni ya kipekee , ili maendeleo yaweze kupatikana lazima sayansi na Teknolojia ihusike” anasema Mchechu

Anazidi kueleza kuwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina inaangalia namna ya kuanzisha kitengo kitakachounganisha watafiti, uhamasishaji rasimali na ubiasharishaji ili kuwezesha tafiti zinazofanyika kuwafikia walengwa hivyo kukuza uchumi wa Taasisi na nchi.

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, ziara ya Msajili wa Hazina ni muendelezo katika kuleta mageuzi ya kiutendaji katika taasisi za umma ikiwemo taasisi ya Nelson Mandela ambayo ni kiota cha sayansi , teknolojia na ubunifu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi ndani na nje ya nchi kupitia bunifu zake.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu alipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Kituo cha Elimu Kuditali (C-CoDE) maktaba, Maabara, kituo cha tehama (HPC),kituo Atamizi (Incubation Centre), Kiwanda kidogo (DDI) pamoja na mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Henry Kahimba (Kushoto) alipotembelea Maabara ya Taasisi hiyo.

Msajili ya Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (aliyekaa) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Bw. Octavian Kanyengele ( kushoto) namna elimu kidigitali inavyotolewa katika kituo cha elimu ya kidigitali ( C-CoDE) kilichopo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Oktoba 21, 2024 kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof Maulilio Kipanyula.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (katikati) akipata maelezo kuhusu mashine ya kisasa ya kuchakata uchafu na kuzalisha mbolea na gesi asilia kutoka kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Petro Mwamlima (kulia) katika kituo cha Atamizi Oktoba 21, 2024, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilo Kipanyula.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Msaidizi wa Chakula na Lishe Kelvin Vulla (Kushoto) wakati alipotembelea kiwanda kidogo cha DDI Oktoba 21, 2024 kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (wa pili kulia) akisisitiza jambo alipotembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Oktoba 21, 2024 , wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof Maulilio Kipanyula, Meneja Milki Ing. Willyhardus Karumuna ( wa kwanza kushoto) .

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (kushoto) akipata maelezo kuhusu bunifu ya funza lishe kutoka kwa Mtafiti Dkt Aziza Konyo ( kulia) alipotembelea kituo Atamizi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (mwenye suti ya bluu) akimsikiliza Mtafiti wa Ngwara ambaye ni Mhadhiri Dkt. Pavithravani Venkataramana alipotembelea kituo Atamizi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Oktoba 21, 2024.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakati wa ziara ya kikazi Oktoba 21, 2024.

Related Posts