DKT. YONAZI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, Dkt. Yonazi yupo nchini Namibia kwa ajili ya kushiriki Kikao cha Tisa cha Jukwaa la Kanda la Afrika la Kupunguza Athari za Maafa na Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Viongozi (High Level Meeting) kuhusu masuala ya kupunguza athari za maafa vinavyofanyika Windhoek nchini Namibia. Mikutano hiyo inafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 24 Oktoba, 2024.
Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Namibia Bw. Elias Tamba akizungumza jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi alipotembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia tarehe 23 Oktoba, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Namibia Bw. Elias Tamba aliptembelea Ofisi za Ubalozi huo kisha kushiriki Kikao cha Tisa cha Jukwaa la Kanda la Afrika la Kupunguza Athari za Maafa na Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Viongozi (High Level Meeting) kuhusu masuala ya kupunguza athari za maafa vitakavyofanyika Windhoek nchini Namibia. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Namibia Bw. Elias Tamba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Menjimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Brig. Jenerali Hosea Ndagala (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Charles Msangi alipotembelea katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Namibia.

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Brig. Jenerali Hosea Ndagala akizungumza jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi nje ya ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Namibia walipotembelea tarehe 23 Oktoba, 2024, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi na wa pili kushoto ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. January Kitunsi.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Related Posts