HALI YA WATOTO NA BIASHARA BADO NI MBAYA NCHINI : JAJI MSTAAFU MWAIMU

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mwaimu akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara uliofanyika leo Oktoba 23,2024 Jijini Dodoma. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Flanklin Rwezimula akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara uliofanyika leo Oktoba 23,2024 Jijini Dodoma. 

Viongozi na wadau katika mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara uliofanyika leo Oktoba 23,2024 Jijini Dodoma. 

Picha ya pamoja kati ya Viongozi na wadau katika mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara uliofanyika leo Oktoba 23,2024 Jijini Dodoma. 

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema hali ya watoto na biashara bado ni mbaya jambo lililopelekea kuingizwa katika mpango kazi wa haki za binadamu na biashara.

Jaji Mstaafu Mwaimu ameyasema hayo leo Oktoba 23,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa kitaifa wa wadau wa haki ya mtoto katika biashara huku akiongeza kuwa watoto bado wanatumikishwa katika biashara hasa katika migodi na kwenye mashamba makubwa.

“Ndiyo maana tumeona wanastahili nawenyewe kuingizwa kwenye huu mpango kazi wa haki za binadamu na biashara na inafanyika hivyo kwasababu nadhani bado mnatambua kwamba watoto bado wanatumikishwa katika biashara hivyo eneo hili kufanyiwa kazi ni sehemu ya mkakati ambao utasaidia na baada ya mpango kazi huu kuandaliwa panaweza kuwa na masuala ya elimu kwa wafanyabiashara ili waweze kuona umuhimu wa kutokuajili watoto,”amesema.

Amesema mtoto kufanya kazi ni haki yake ya msingi lakini sio zile kazi ambazo zinawaumiza watoto na kuwaacha na majeraha.

Awali akifungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Flanklin Rwezimula amewaomba washiriki kushiriki katika mdahalo kikamilifu na kuongeza kuwa mipango na mikakati maalum ya kumlinda mtoto inajumuisha mpango kazi wa kuondoa ajira mbaya ya mtoto pamoja na muongozo wa uendeshaji wa mashauri ya ulinzi wa haki zake.

“Niwaombe kushiriki vyem katika mdahalo huu kikamilifu ili kuwezesha kutambua ombwe zitakazo saidia kuweka mikakati, Mipango na kutenga rasilimali fedha za utekelezaji wa haki ya mtoto katika biashara,”amesema.

Sanjari na hayo ameihakikishia THBUB kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao iliniweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndogondogo Mkoa wa Dodoma kupitia Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA), Christian Msumari amekiri kuwa changamoto hiyo ipo katika maeneo yao na watoto wanakumbana na mazingira magumu.

“Mimi kama kiongozi ambaye nipo kwenye nyaja ya biashara na wafanyabiashara ndogondogo hiyo naomba nikiri kweli hiyo changamoto ipo katika maeneo yetu ya masoko na maeneo yetunya biashara kwasababu kwenye haya maeneo watu wengi wenye kipato kidogo wanaingia kwasababu nisamehemu ambayo inaruhusu watu wote kuingia na hazina makatazo,”amesema.

Amsema namna ambavyo watoto wadogo wanaingia na mazingira wanayokutana nayo sio rafiki kulingana na umri walionao na waliyolelewa na kukutana na watu mbalimbali wenye tabia tofauti hivyo wanajikuta wanaingia kwenye mfumo wa malezi ambao sio rasmi.

Pia nae, Mratibu wa Chama Cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA), Neema Ahmed amesema wao kama wadau watoa msaada wa kisheria wanachangia katika mpango huo ili kuona ni namna gani utaboresha upatikanaji wa haki za watoto hususani wale wanajishughulisha na kazi.

Related Posts