Ameyasema hayo leo tarehe 22/10/2024 wakati wa ufunguzi rasmi wa warsha ya Kimataifa wa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) katika Hotel Seascape, Dar es salaam iliyoratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe na kushirikisha nchi ambazo zimezunguka Ukanda wa bahari ya Hindi
Naibu Waziri Khamis, ametoa rai kwa wadau wote wa ukanda wa bahari ya Hindi (IORA), kuhakikisha kwamba jamii inapata uelewa na elimu sahihi ya kuhusu kutunza Mazingira
“Kwetu sisi wasomi twendeni tukatoe elimu kwa jamii kuhusu kutunza Mazingira, jamii yetu haina uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Ikolojia, kaboni na namna bora ya utunzaji wa mazingira twende tukawaelimishe watu jinsi ya kuvuna kaboni” alisisitiza Mhe Khamis.
Amesema uelewa wa masuala ya Kaboni na matumizi sahihi ya rasilimali za bahari kupitia uchumi wa bluu ni muhimu kwa jamii inayozunguka mazingira ya pwani kwa kuwa husaidia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa kwa Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA) kuweka nguvu zaidi katika kutoa elimu. “Tunaomba mtusaidie kuelimisha jamii ili kutunza Mazingira.”Alisitiza Mhe Khamis
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema wakati ni sasa wa kuunganisha nguvu za wasomi, watafiti na wanamazingira kuendelea kuhimiza uhifadhi wa mazingira na kusisitiza matumizi sahihi ya uchumi wa bluu kama njia ya kulinda mazingira na chanzo cha maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo.
Nchi au ukanda unaohusishwa na IORA (Indian Ocean Rim Association – Jumuiya ya Ukanda wa Bahari ya Hindi) umeanza kugundua na kutumia faida za “kaboni ya bluu” katika juhudi zao za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa njia endelevu. Alifafanua Prof.Mwegoha.
Naye mratibu wa warsha hiyo Dkt. Saida Fundi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe amepongeza IORA na kuelezea namna inavyo pambana kutunza Mazingira na kuelimisha jamii kwa ujumla.
“Ni muhimu jamii ikaelimika na kuwa na uelewa mpana juu ya mazingira ili iwe rahisi kuyatunza na kuhifadhi kwa maendeleo ya vizazi vijavyo” amesisitiza Dkt. Saida
Mkutano huo umejumuisha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali kutoka ukanda wa bahari ya buluu ikiwa ni pamoja na Australia, Bangladesh, Comoros, France, India, Indonesia, Iran, Kenya, Madagascar, Malaysia, Maldives, Mauritius, Mozambique, Oman, Seychelles, Singapore, Somalia, South Africa, Sri Lanka, Tanzania, Thailand, United Arab Emirates, Yemen.