KAMATI YA BUNGE YAPOKEA TAARIFA YA MITAMBO YA KISASA YA UCHIMBAJI VISIMA

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira inayoongozwa na mwenyekiti
Jackson Kiswaga imepokea taarifa kuhusu matumizi ya mitambo ya kisasa 25 ya kuchimba visima.

Taarifa hiyo imetolewa Jijini Dodoma ambapo imehusu pia visima na hatua iliyo fikiwa katika usambazaji wa maji ya visima na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Mitambo hiyo ya kisasa ilitolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma ya majisafi inaimarika nchini.

Taarifa kuhusu mitambo hiyo imeeleza namna inavyojenga weledi na ufanisi kwa wataalam pamoja na watendaji wengine katika kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa kutumia teknolojia na vifaa vya kisasa

Mafanikio yaliyopatikana katika uchimbaji wa visima ni pamoja na kuchimba na kuendeleza idadi ya visima 650 katika vijiji 876 na kunufaisha zaidi ya wananchi milioni sita.




Related Posts