MATAIFA ZAIDI YA 22 WASHIRIKI MAONESHO YA MAFUTA NA GESI JIJINI DAR

 Mkurugenzi wa ldara ya Uhamasishaji na Uwezeshaji Uwekezaji, Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA), James Maziku akikata utepe kuashila uzinduzi wa mafuta na gasi yanayofanyika katika ukumbi wa Daimondi Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa ldara ya Uhamasishaji na Uwezeshaji Uwekezaji, Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA), James Maziku akizungumza wakati wa kuzindua maonesho ya mafuta na gasi yanayofanyika katika ukumbi wa Daimondi Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa AUTO EXPO AFRICA Group, Duncan Njage akizungumza wakati wa uzinduza maonesho ya mafuta na gasi yanayofanyika katika ukumbi wa Daimondi Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa ldara ya Uhamasishaji na Uwezeshaji Uwekezaji, Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA), James Maziku akipata maelezo katika mabanda mbalimbali leo Oktoba 23, 2024 jijini Dar es Salaam.

MATAIFA zaidi ya 22 duniani wameshiriki maonesho Mafuta na gesi yaliyoandaliwa na kampuni ya Auto Expo Africa 2024 yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kuanzia leo Oktoba 23- 25, 2024.

Mkurugenzi wa ldara ya Uhamasishaji na Uwezeshaji Uwekezaji, Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje(EPZA), James Maziku akizungumza wakati wa kufungua maonesho hayo leo Oktoba 23, 2024. Amesema kuwa katika maonesho hayo ni katika mnyororo wa thamani wa sekta ya mafuta na gesi katika usambazaji.

“Katika maonesho haya kuna bidhaa nyingi ambazo zinaonesha teknolojia ya hali ya juu kwaajili ya kujifunza katika uzalishwaji wa Mafuta na gesi hapa nchini.

Pia Maziku amesema kuwa katika mnyororo wa dhamani bado kuna teknolojia ambazo zitasaidia Tanzania kuwa kitivo cha Uzalishaji, usambazaji na masoko yaliyopo karibu.

“Maonesho kama haya ni njia rahisi yenye gharama nafuu katika kuvutia wawekezaji nchini.

Ni wakati muafaka wa kupanua wigo wa kuvutia wawekezaji katika mataifa mengi yaliyokuja katika maonesho haya.” Ameeleza

Ameleza kuwa Tanzania inanafasi ya pekee kuvutia wawekezaji kulingana na mazingira, sera na sheria za uwekezaji zilizopo.

Maziku ameeleza kuwa amani iliyopo katika maeneo ya kisiasa na kijamii Tanzania bado inaonekana ipo imara.

“Tunatarajia maonesho kufanyika kwa wingi hapa nchini ili watu wanaokuja katika maonesho waelimike na waone fursa hapa hapa nchini.” Amesema Maziku

Akizungumzia kuhusiana na sera na sheria za hapa nchini amesema kuwa zipo wazi wawekezaji wote wanaokuja nchini kwa mujibu wa sheria na wanafata sheria zote za nchi kuanzia sheria za mazingira, Ardhi, ajira, kazi na afya.

Amesema maonesho hayo yatapelekea watanzania baada ya miaka mitano ijayo kuwa na teknolojia ambayo wameiona katika maonesho hayo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa AUTO EXPO Group, Duncan Njage amewakaribisha watanzania kujionea teknolojia mpya zinazo oneshwa katika maonesho ya 24 ya AUTOEXPOAFRICA 2024 yanayofanyika Diamod Jubilee jijni Dar es Salaam.

“Hapa kunateknolojia nyingi za Uzalishaji na uchakataji wa Mafuta na gesi.” Amesema

Related Posts