MFUMO WA IFTMISS KUTUMIKA NCHI NZIMA KABLA YA JULAI 2025

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI, Ndg. Sospeter Mtwale amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha mfumo IFTMIS (Inspection and Finance Tracking Management Information System) utakuwa ukitumika nchi nzima kabla ya Julai 2025 ili kurahisisha Ukaguzi na Ufuatiliaji wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Ndg. Mtwale ameyasema hayo leo tarehe 23/10/2024 wakati akifungua mafunzo ya mfumo huo kwa watumiaji wa ngazi ya Sekretarieti za Mikoa yalioyohudhuriwa na Makatibu Tawala Wasaidizi (Menejimenti, Ufuatiliaji na Ukaguzi), Maafisa TEHAMA wa Mikoa na Wakaguzi wa Ndani wanaoshughulikia Halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa VETA Jijini Dodoma.

“Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mfumo imekamilika. Hatua inayofuata kwa sasa ni mafunzo kwa watumiaji wa Mfumo ambapo Serikali imeanza na Wataalamu kutoka Ofisi za Wakuu wa Mikoa na baadae yatafanyika kwa Wataalamu kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa”.

Amesema Mfumo wa Kielekroniki wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Fedha kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa umelenga kurahisisha Ufuatiliaji kuhusu uzingatiaji Sera, Sheria na thamani ya fedha katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri ikiwemo miradi ya maendeleo,

Pia ameongeza kuwa Mfumo huo utawezeshabUfuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi mbalimbali, ikiwemo ukaguzi wa CAG na Maagizo ya Kamati ya Bunge ya LAAC pamoja Ufuatiliaji wa makusanyo, mapokezi na matumizi ya fedha kwenye Halmashauri








Related Posts