SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI ILI KUKUKUZA UCHUMI WA NCHI.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akihutubia wananchi wa Jiji la Mbeya, wakati akifungua Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambapo aliagiza Watoa huduma za Fedha kuendelea kutekeleza majukumu yao kulingana na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa 2021/22-2025/26, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2021/22-2029/2030 na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (5) wa Elimu ya Fedha (2019/20-2025/26) kwa ajili ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha na Nchi kwa ujumla.

Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (Kulia) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yaliyofunguliwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya.

Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mbeya, wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Hayupo Pichani), wakati akifungua Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Kushoto), akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama Mkuu kutoka Idara ya Menejimenti ya Mifumo ya Kifedha, Bw. Frank Kanani, kuhusu Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG), wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Kulia), akielekezwa na watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), namna ya kuhakiki taarifa za wastaafu, wakati alipotembelea Banda la Mfuko huo wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Katikati), akimsikiliza mmoja wa Wajasiriamali kutoka kikundi cha wajasiriamali wadogo cha Tanzania Informal Microfinance Associations of Practitioners (TIMAP), Bi. Tamasha Juma Ngunda (Kushoto), wakati alipotembelea Banda la wajasiriamali hao, wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimuwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Kulia ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja.

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Katikati aliyeketi), akiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wa sekta ya fedha (Regulators), baada ya hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimuwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Wengine katika picha ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (watatu kulia), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Kayuni (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Bw. Beno Malisa ( wa tatu kushoto ) na viongozi wengine.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Katikati aliyeketi), akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yaliyofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambapo katika halfa hiyo alimuwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Wengine katika picha ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (watatu kulia), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Kayuni (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Bw. Beno Malisa (wa tatu kushoto ) na viongozi wengine. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mbeya).

……….

Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Mbeya

Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 133.310 kwenye sekta ya wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwawezesha mitaji, kutoa mafunzo ya ujasiriamali, matumizi ya huduma za fedha, tafiti kuhusu sekta ya fedha na kuongeza matumizi ya TEHAMA kwenye sekta ya fedha.

Hayo yameelezwa jijini Mbeya na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya.

Alisema Serikali imepanga kutekeleza hayo katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa 2021/22 -2025/26 ambapo wahusuka wakuu ni Taasisi za Fedha na watoa huduma za Fedha.

”Watoa huduma za Fedha watekeleze majukumu yao kulingana na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa 2021/22-2025/26, Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha 2021/22-2029/2030 na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (5) wa Elimu ya Fedha (2019/20-2025/26) kwa Maendeleo ya Sekta ya Fedha na Nchi kwa ujumla” aliagiza Prof. Mkenda.

Alisema Serikali imekuwa ikiboresha Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Fedha kwa lengo la kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja.

Mhe. Prof. Mkenda alisema katika jitihada hizo Serikali imefanikiwa kuongeza mchango wa Sekta ya Fedha katika ukuaji wa uchumi pamoja na kuongeza upatikanaji na utumiaji wa huduma jumuishi za fedha kutoka asilimia 65 mwaka 2019 hadi asilimia 76 mwaka 2023.

Aidha, alitaja mafanikio mengine kuwa ni watoa huduma Ndogo za Fedha kutambuliwa, kusajiliwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, kuongezeka kwa upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na kuimarika kwa utamaduni wa kujiwekea akiba.

Alitumia fursa hiyo kuipongeza Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau wa Sekta ya Fedha kwa kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha wananchi kutumia huduma rasmi za fedha, ambapo jumla ya Mikoa 12 na Halmashauri 65 na wananchi zaidi ya 32,000 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Mei, 2024 hadi Septemba, 2024 walifikiwa.

Aidha, alisema mtaala mpya wa elimu umejumuisha elimu kuhusu fedha kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ambapo utekelezaji wake masomo yanahusu masuala ya fedha na ujasiriamali yatakua ya lazima.

Kwa upande wake, Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja alizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alisema Sekta ya Fedha ni miongoni mwa sekta muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Alisema Sekta hiyo, pamoja na mambo mengine ina majukumu mbalimbali ikiwemo kutoa taarifa za masoko, kuhamasisha kuweka akiba na kuwezesha kuuza na kununua bidhaa, uwekezaji na mitaji, kuwezesha biashara, kuweka utaratibu mzuri wa kushughulikia vihatarishi katika sekta ya fedha, kujipanga na maisha ya uzeeni pamoja na kuelimishwa umma kuhusu masuala ya bima.

Dkt. Mwamwaja alisema kuwa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa itafanyika kwa umahiri mkubwa na anatarajia kuea mwisho wa madhimisho hayo yatawezesha malengo ya Wiki hiyo yatafikiwa kama ilivyokusudiwa.

Related Posts