WALEMAVU WA MACHO WAPEWE FURSA KAMA WATU WENGINE

Na Linda Akyoo -Moshi

Mratibu wa Chama cha Wasioona Tanzania kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira vijana na wenye ulemavu Kizito Lucas Wambura,amefanya ufunguzi rasmi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe,na miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.Huku lengo kuu la kongamano hilo likiwa ni kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kutambua na kusaidia watu wenye ulemavu wa macho.

Bw.Wambura ameyasema hayo leo tarehe 23 Oktoba,2024,akisisitiza umuhimu wa kushirikiana kama jamii ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wa macho wanapata huduma bora na fursa za maendeleo.

Aidha Wambura aliongeza kwa kusema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira vijana na wenye ulemavu itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wa maendeleo kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata haki zao za msingi.

Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Wasioona Tanzania Bi.Habiba Salum Ngulangwa ameielimisha jamii juu ya changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa macho ikiwa ni pamoja na ajira na jinsi wanavyoweza kusaidiwa. Hata hivyo alisema kuwa washiriki watapatiwa elimu kuhusu mbinu za kuwasaidia ili waishinkama watu wasio na ulemavu na kuwa na maisha bora.

Kwa upande wake Bw.Michael Mashauri ambe ni mshiriki kwenye kongamano hilo ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira vijana na wenye ulemavu pamoja na kamati ya maandalizi kwa kuandaa mada zitakazo wafanya waweze kujitegemea,Ameongeza kwa kusema kuwa watu wenye ulemavu ni msaada kwa Tanzania kwani kuna waliopanda mlima Kilimanjaro kwaajili ya kuipandisha fimbo nyeupe kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuutangaza utalii wa ndani na kuchangia juhudi za Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kongamano hilo lilikuwa ni hatua muhimu katika kuelimisha jamii na kuhamasisha juu ya umuhimu wa kusaidia watu wenye ulemavu wa macho,na lilienda sambamba na kauli mbiu isemayo “Upatikanaji wa Teknolojia Saidizi na Fikivu ni Mkombozi kwa Mtanzania Asiyeona”,kilele cha kongamano hilo ni Tarehe 25 Oktoba,2024.

Related Posts