Benki ya Absa Tanzania yahitimisha wiki ya huduma kwa wateja ikiahidi huduma bora zaidi kwa wateja wake

Wakati Benki ya Absa Tanzania ikihitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kukutana na wateja wake katika hafla maalumu jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Obedi Laiser amesema tukio hilo ni ishara ya shukrani kwa wateja wao waaminifu huku ikitambua mchango wao muhimu katika ukuaji na mafanikio ya benki hiyo kwa miaka mingi.

“Wateja wetu ndio moyo wa kila tunachofanya,” alisema Bw. Laiser. “hafla hii ya kifungua kinywa ni ishara ndogo ya shukrani yetu kwa imani na uaminifu mliotuonesha. Kama benki, tumejikita kikamilifu kutimiza ahadi zetu kwa kutarajia na kukidhi mahitaji yenu katika kila hatua. Msaada wenu wa kuendelea umekuwa msingi wa mafanikio yetu, na tutaendelea kujitahidi kufanya zaidi ya matarajio yenu.”

Hafla hii ilifanyika sambamba na hitimisho la Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambayo iliadhimishwa chini ya kaulimbiu ya (Above and Beyond) “Zaidi ya Matarajio.” Kaulimbiu hii inahusiana kwa karibu na kujitolea kwa Benki ya Absa Tanzania kuvuka matarajio ya wateja na kutoa huduma bora. Bw. Laiser alithibitisha tena dhamira ya benki hiyo ya kutoa uzoefu wa wateja ulio bora, wenye ufanisi, na unaozingatia mahitaji ya kibinadamu, kwa kufanya zaidi ya matarajio katika kukidhi mahitaji ya kifedha ya sasa na ya baadaye.

“Katika Absa, tumejikita katika kutoa viwango vya juu vya huduma. Uhakika, ufanisi, faragha, na uadilifu ni nguzo kuu zinazotuongoza katika uzoefu wa wateja wetu. Wafanyakazi wetu ndio msingi wa dhamira hii, na tunawekeza katika maendeleo yao ili kuhakikisha tunatoa huduma bora kila mara. Tunafanya kazi kama timu moja, tukiwazingatia wateja wetu katika kila tunachofanya.”

Alisisitiza zaidi kwamba benki inajitahidi kutoa huduma makini, inayofika kila mahali, na isiyo na makosa, huku ikihakikisha wateja wanapewa taarifa katika kila hatua. Katika matukio nadra ambapo matarajio ya huduma hayafikiwi, benki inaahidi kurekebisha hali hiyo haraka, ikionyesha zaidi msimamo wake wa kuweka wateja mbele.

Lengo la Benki ya Absa, “Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine, na ahadi ya chapa yake, “Stori yako ina thamani,” pia ilielezwa kwa ufasaha wakati wa hafla hiyo. Bw. Laiser alieleza jinsi benki hiyo inavyolenga kuunda uzoefu unaozingatia kibinadamu unaoakisi Stori binafsi za wateja wake. Alisema stori hizi zinaihamasisha benki hiyo kuendelea kuboresha viwango vyake vya huduma, kuhakikisha kila mwingiliano unakidhi mahitaji ya wateja huku ikitarajia malengo ya kifedha ya baadaye.

“Stori zenu zinatuvutia kufanya zaidi ya matarajio katika kila tunachofanya,” alisema Bw. Laiser. “Katika Absa, tunaamini kila mteja ana Stori ya kipekee, na Stori hizi zinatuhamasisha kutoa uzoefu wa kibenki unaolengwa, unaozingatia huruma, na unaolenga kutoa suluhisho sahihi za kifedha.”

Kama sehemu ya jitihada za benki hiyo za kuendelea kujihusisha na wateja na kuwazawadia kwa uaminifu wao, Benki ya Absa Tanzania pia ilitumia fursa hiyo kuwakumbusha wahudhuriaji kuhusu kampeni yake inayoendelea ya “Spend & Win.” Kampeni hiyo, ambayo iko wazi kwa wateja wote binafsi, inawapa washiriki nafasi ya kushinda Subaru Forester ya mwaka 2014 na zawadi nyingine za kusisimua. Droo ya kwanza ilifanyika Oktoba 22, 2024, na benki ilikuwa na furaha kutangaza kuwa mshindi tayari amechaguliwa, huku hafla ya utoaji wa gari ikitarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kampeni ya “Spend & Win” inahimiza wateja kuendelea kutumia kadi zao za Absa na njia za kibenki za kidigitali kwa miamala yao, na kuwapa nafasi zaidi za kushinda katika droo zijazo.

Akihitimisha hafla hiyo, Bw. Laiser alisisitiza tena ahadi ya benki hiyo ya kuwawezesha wateja wake na kuhakikisha wanahisi kuthaminiwa katika kila hatua: “Tutaendelea kusikiliza mahitaji yenu na kutoa suluhisho zitakazowawezesha kufikia malengo yenu ya kifedha. Pamoja, tunajenga Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (Metl ), Vipul Kakad ( wa pili kushoto) katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja, jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Metl, Shamma Dhrani na Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa benki hiyo, Nellyana Mmanyi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser akihitimisha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Tigo, John Sicilima ( katikati ) katika hitimisho la wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki hiyo, Oscar Mwamfwagasi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Tanganyika Christian Refugee Service, Irene Mpangile (katikati) katika hafla ya kuhitimishs maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo, Melvin Seprapasen.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Absa Tanzania, Eveline Kamara akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA, Eric Sambu, wakati wa hafla ya hitimisho la wiki ya huduma kwa wateja iliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Ofisa Manunuzi wa benki hiyo, Ikunda Kishimbo.

Related Posts