REA kupeleka nishati ya umeme kisiwa cha Izumacheli kilichopo ndani ya ziwa victoria.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Geita tayari wamepeleka Huduma ya Nishati ya Umeme katika Vitongoji 1017 kati ya Vitongoji 2195 vya Mkoa wa Geita ambapo Kata Moja ya Izumacheli yenye Vijiji vitatu vya Izumacheli ikiwemo Butwa na Lunazi bado havijafikiwa na Umeme kutokana na kata hiyo kuwa ndani ya Ziwa Victoria huku matarajio ikiwa ni kukifikia kIsiwa hiyo.

Hayo yameelezwa na Msimamizi REA Mkoa wa Geita , Mhandisi , Dominick Mnaa wakati akitoa Taarifa fupi ya Utamburisho wa Mkandarasi wa Mradi wa Upelekaji Umeme Vitongoji (HEP) Mkoani Geita Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa huo Martine Shigela ambapo wametaja sababu ya kutofikiwa umeme kutokana na Vijiji hivyo kuwa Visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria.

“Hali ya umeme katika Mkoa wetu wa Geita Mkoa wa kwanza Geita unajumla ya Kata 122 , Vijiji 486 na Vitongoji 2195 mpaka tunapoongea leo Jumla ya kata 121, Vijiji 483 na Vitongoji 1017 vimekwishakufikiwa na umeme bado vijiji vitatu katika kata moja ya Izumacheli ambayo ipo katika wilaya ya Geita Vijijini hii kata haijafikiwa na Umeme mpaka leo kwa sababu ya kuwa na ipo kwenye Visiwa ndani ya Ziwa Victoria , ” Mhandisi Msimamizi REA Mkoa wa Geita, Bw.Mnaa.

“Leo tumekuja na Mkandarasi huyu ambaye anakuja kutuanzishia safari ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 105 vya mkoa wa Geita ambapo Geita tuna Jumla ya majimbo saba ambapo kila jimbo lina vitongoji 15 hivyo kutengeneza jumla ya vitongoji 105 mradi huu unatarajia kuchukua siku 730 ambayo ni sawa sawa na Miaka miwili ikianzia leo na Mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 17.77, ” Mhandisi Msimamizi REA Mkoa wa Geita ,Bw. Mnaa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 17.77 huku akiwataka REA kuhakikisha inafikisha Umeme katika Kata ya Izumacheli yenye Vijiji viwili ambavyo viko ndani ya ziwa Victoria ambavyo vimechukua muda mrefu kutokana na sababu hizo.

“Maana ya kwamba kila Jimbo kutapelekewa Umeme kwenye Vitongoji 15 kwahiyo 15 mara saba unapata Jumla vitongoji 105 na Mradi huu ni mradi ambapo Serikali ya Dkt.Samia imeshatoa Fedha zaidi ya Bilioni 17 ambazo zitapeleka umeme kwenye vijiji vyetu lakini vilevile mradi huu utatumia miaka miwili kuhakikisha kwamba umeme maeneo yote yameelekezwa upatikaniji wa umeme unapatikana kwa wakati , ” Mkuu wa Mkoa wa Geita, Shigela.

“Nafarijika kuona kwamba REA wamejipanga vizuri wamekuja kunitambulisha mkandarasi na nimatumaini yetu kwamba viongozi wetu kule ambako umeme utakapopelekwa kwenye vitongoji watakwenda kutoa ushirikiano unao staili najua taratibu za REA na taratibu za TANESCO huwa hazina Fidia mahala ambapo nguzo zinawekwa ni wajibu wa viongozi wa Vitongoji , Vijiji , Mtaa kuhakikisha suala la kuwasaidia wakandarasi na REA kupitisha nyaya za umeme ili waweze kupata umeme ni suala ambalo watawajibika , ” Mkuu wa Mkoa wa Geita, Shigela.

Related Posts