Ukosefu wa taulo za kike ni changamoto kwa wanafunzi

Ukosefu wa taulo za kike hususani kwa wanafunzi wanaotoka katika kaya masikini ni miongoni mwa changamoto zinazochangia baadhi yao kushindwa kuhudhuria masomo kwa kipindi chote cha hedhi hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao kulinganisha na wengine wenye uwezo.

Kufuatia hali hiyo Kampuni ya Beneficia imeamua kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari ya Osterbay iliyopo Jijini Dar es salaam ikiwa ni mpango wa kuiunga mkono serikali ambayo inafanya jitihada kubwa za uwekezaji wa miundombinu ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata haki yake ya msingi ya kupata elimu katika mazingira bora na Rafiki.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja mauzo wa Beneficia Perepetua Mwatle,amesema kuwa kuna baadhi ya mabinti na watoto wanaotoka familia za chini na duni ndio wenye mahitaji maalumu kwani kukosa masomo kisa taulo za kike ni jambo lisilikubaliwa kabisa.

 

Imebainika kuwa baadhi ya makabila yamekuwa na mila ambazo hazitoa mwanya wa kuzungumzia masuala ya hedhi salama yakiamini ni kinyume na utaratibu hivyo kuifanya jamii kukosa elimu sahihi juu ya masuala ya afya ya uzazi.

 

 

Ayotv imezungumza na wanafunzi Pamoja na walimu licha ya kupokea taulo za kike kutoka Manispaa wamekiri kuwa wapo baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka katika mazingira magumu ambao hukabiliwa na changamoto ya kukosa taulo za kike wakati wa hedhi.

 

Hayo yamesemwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Osyterbay Meridah John wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuelezea namna wanafunzi wanavyokosa masomo kisa changamoto ya kukosa taulo za hedhi kwani familia zao hazina uwezo wa kupata huduma za taulo hizo,pia wameishukuru Beneficia kwa kuwaletea msaada wa taulo hizo na pia kuwapatia elimu kuhusu matumizi ya taulo hizo za hedhi.

Related Posts