KAMPENI YA TUWAAMBIE KABLA YA HAWAJAHARIBIWA YAENDELEA ARUSHA

Na.Vero Ignatus Arusha.

Jeshi la Polisi wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha limeendelea kutoa Elimu ya kujitambua na namna ya kujiepusha na vitendo via mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo, kujiepusha na makundi na mabaya yatakayoharibu tabia njema na kuingia kwenye upotokaji

Akizungumza leo 25octoba 2024 na wanafunzi Katibu Tawala wilaya ya Arumeru Joseph Mabiti aliwahimiza kujiepusha na mutumizi ya dawa za kulevya, ushawishi utakaopelekea wao kupata mimba za utotoni sambamba kuepuka kuniingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja.

Aidha Mabiti aliitaja mitandao ya kijamii kwamba imekua kichocheo kimojawappo cha kuongezeka kwa matukio ya ukatili, huku akiwageukia wazazi/walezi kujenga
Urafiki na ukaribu na watoto wao,ili waweze kuwasaidia kujiepusha na matumizi mabaya inayopelekea kufanyiwa ukatili

SP Beatrice Mwonga ni Kaimu Mkuu wa Polisi Wilayani humo, amesema lengo la kampeni hiyo ni kuongea na wanafunzi kabla hawajaharibiwa pindi wanapoanza masomo yao katika shule za sekondari na vyuo vikuu kwa mara ya kwanza huku akibainisha kuwa wanaenda kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha tano na vyuo vikuu vyote.

Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limeamua kukutana na makundi hayo katika jamii kuwapa elimu hiyo kwa sababu utandawazi umesababisha mambo yote kuwa hadharani bila ya kificho ambapo wanaenda kuwaelimisha namna bora ya kutumia mitandao hiyo kwa usahihi.

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati katika Wilaya hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Salama Ally amewaeleza wanafunzi hao umuhimu wa kuripoti matukio ya ukatili kwa haraka katika vituo vya Polisi sambamba na kwenda kutoa ushahidi mahakamani pindi watakapohitajika

Itakumbukwa hivi karibuni Jeshi la Polisi lilizindua kampeni ya tuwaambie kabla ya hawajaharibiwa yenye lengo la kuongea na wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu kwa lengo la kuwaelimisha kujitambua ili kuepukana na vitendo vya mmomonyoko maadili.





Related Posts