KAMATI YA BUNGE PIC YARIDHISHWA NA MIRADI YA NHC MTUMBA

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC), imeiomba serikali kuhakikisha inaangalia namna bora ya kuweza kutunza majengo ambayo kwasasa yanaelekea kutamatika ili uwekezaji uliofanyika uweze kuleta tija.

Ombi hilo limetolewa leo Oktba 26,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini Vuma Augustino mara baada ya ukaguzi huo ambapo ameongeza kuwa kwasasa shirika hilo limeirika kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakitimiza wajibu wao.

“Unakuta majengo mengi ya serikali yamejengwa vizuri na yang’aa na yamejengwa kwa mabilioni ya fedha lakini baada ya muda unakuta ni changamoto wanashindwa kuyatunza yanachakaa hasa kwenye miundombinu ya maji taka, muonekano wa jengo lenyewe kwahiyo sisi kama kamati tunaona sasa serikali inapaswa kuanza kuwaza namna ya kuyatunza, “amesema.

Aidha amesema kamati hiyo imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo katika mji wa Kiserikali Mtumba unaotekelezwa na shirika la Nyumba la taifa (NHC).

“Kwanza kamati imeridhishwa na kasinya ujenzi wa majengo yote Nane ambayo NHC wamekabidhiwa kujenga katika mji huu wa serikali Mtumba, kwakweli wamefikia hatua nzuri na miradi mingi ipo jui ya 80% na wanategemea kumaliza ndani ya mkataba waliopewa nasisi tumeona na tumejiridhisha kuwa wanaweza kumaliza ndani ya muda huo,”amesema.

Awali akitoa wasilisho la utekelezaji ujenzi wa majengo ya ofisi za Wizara katika mji wa serikali eneo la Mtumba Jijini Dodoma kwa PIC, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah amesema ili sekta ya Nyumba nchini iweze kupata ustawi mkubwa serikali inapaswa kuendelea kushawishi sera inayoleta unafuu wa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye nyumba za gharama nafuu.

Pia amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la upandaji wa bei vifaa vya ujenzi usio wa kawaida uliotokana na changamoto ya upatikanaji wa dola za kimarekani.

“Changamoto nyingine ni kuchelewa kupata idhini ya dhamana ya serikali kwaajili ya barua ya mkopo toka serikali toka Oktoba 2022 hadi Sep 2023 pamoja na ngezeko la ushuru wa uingizaji wa kodi kwa marumaru na vioo vya madirisha toka 10% hadi 35% ,”amesema.

Related Posts