AWESO AWASHA MOTO BUSEGA,AZINDUA MRADI WA MAJI NA ZAHANATI NA KUAHIDI MIL.40

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amezungumza na wananchi Shigala wilayani Busega mkoani Simiyu na kuwaeleza dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuwaletea maendeleo chini ya uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Waziri Aweso amezindua Mradi wa Maji Kabita wa kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5.

Pia Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuhakikisha Shillingi Milioni 40 kuendeleza kazi ya kuwapatia wananchi wa Shigala Maji baada ya kazi ya kuchimba kisima kukamilika.

Awali Waziri Aweso amezindua mradi wa jengo la Zahanati ya Milambi ikiwa yote hii ni muendelezo wa ziara maalumu inayohusisha kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua na kuzindua Miradi ya Maendeleo ya sekta mbalimbali sambamba na kuzungumza na wananchi wa wilaya zote za mkoa huu kwaniaba ya Mhe Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Related Posts