Urusi yasema imedhibiti kijiji kimoja mashariki mwa Ukraine – DW – 27.10.2024

Urusi imesema wanajeshi wake wamesogea zaidi mashariki mwa Ukraine na kukitwaa kijiji kimoja kwenye eneo la mapambano, kilomita chache tu kutoka kaskazini mwa mji muhimu ambao ni kitovu wa shughuli za kiviwanda unaoshikiliwa na Ukraine.Soma Pia: Viongozi wakuu duniani waunga mkono uhuru wa Ukraine

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimelikombowa eneo la makaazi la Izmailovka, ambalo kimsingi ni kijiji kwenye mji wa Izmailivka.

Moscow imepiga hatua ya kusonga mbele katika mapambano hayo kwa kipindi cha miezi kadhaa, ikionesha kupata mafanikio dhidi ya vikosi vya Ukraine vilivyozidiwa nguvu.

Mji wa Izmailivka ulikuwa ukikaliwa na idadi ya watu chini ya 200 kabla ya vita hivyo vya Urusi na unakutikana kilomita nane kutoka Kaskazini kwa mji muhimu wa Kurakhove wenye shughuli za Kiviwanda na ambao pia uko kaskazini mwa Kurakhivka,mji mdogo ulioko kwenye eneo la mapigano ambako Urusi inajaribu kuzingira.

Mji wa Belgorod ulivyoharibiwa
Mashambulizi ya maroketi BelgorodPicha: Belgorod Region Governor Vyacheslav Gladkov Telegram channel/AP/picture alliance

Tangazo la Urusi limekuja saa chache baada ya kudai kudunguwa droni 51 za Ukraine zilizorushwa kwenye maeneo mengi ya majimbo yake ikiwemo karibu na mpakani.

Leo Jumapili pia rais Vladmir Putin ameonya kwamba nchi yake itajibu ikiwa mataifa ya Magharibi yatairuhusu Ukraine kutumia silaha za mataifa hayo za masafa marefu kushambulia kwenye ardhi yake.Soma pia: Kansela Olaf Scholz wa ujerumani ahofia kutumwa wanajeshi wa Korea kaskazini nchini Ukraine

Putin alitowa onyo hilo kupitia televisheni ya taifa pale alipoulizwa na mwandishi mmoja wa habari.Alisema ni mapema kutowa uamuzi lakini bila shaka idara ya ulinzi inafikiria kuhusu suala hilo na itatowa mapendekezo kadhaa ya  mwelekeo wa kuchukuwa. 

Kilio cha Zelensky

Ama kwa upande wake Ukraine,rais Voloymyr Zelensky leo Jumapili amerudia tena mwito wake kwa washirika wake wa nchi za Magharibi wa kutaka wamsaidia na zana za ulinzi wa anga.

Rais  Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine-Volodymyr ZelenskyPicha: Ukraine Presidency via Bestimage/IMAGO

Kupitia ukurasa wa X kiongozi huyo wa Ukraine ameandika kwamba ndani ya kipindi cha wiki moja iliyopita pekee Urusi imefanya mashambulio 1,100 dhidi ya nchi yake ikitumia mabomu yanorushwa kwa kutumia miamvuli na zaidi ya mashambulizi 560 ya droni.

Kwa mujibu wa Zelensky wanajeshi wa Urusi pia walifyetuwa kiasi maroketi 20 na makombora ya masafa marefu dhidi ya nchi yake na kutokana na kuzidi kwa mashambulizi hayo,anahitaji msaada wa kuwalinda wake.

Amesisitiza kwamba ushirikiano na washirika wake wa Magharibi unaendelea, lengo likiwa ni kukomesha ugaidi unaoendeshwa na adui,Urusi.

 

Related Posts