JUNGULU ATEMA CHECHE AWATAKA WANA CCM KUUNGANA NA KUVUNJA MAKUNDI

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Picha ya ndege iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha mji Grace Jungulu amewahimiza wanachama wote kuhakikisha kwa sasa wanavunja makundi yote na kuungana kwa pamoja na kueleleza nguvu ili kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mtaa.

Jungulu ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa ccm ikiwa ni baada ya kumalizika kwa zoezi la kura la maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea ambao watakiwakilisha chama katika uchaguzi huo.

Alisema kwamba mchakato wa kura za maoni umeshafanyika na kumalizika hivyo.mgombea ambaye atakwenda kukiwakilisha chama wa CCM inapaswa apewe ushirikiano wa kutosha na kuweka kabisa tofauti ambazo zilikuwepo hapo awali kwani wote lengo ni moja katika kukijenga na kikiimarisha chama.

“Kwa kweli mimi ninashukuru Mungu kama Mwenyekiti tumeweza kushirikiana bega kwa bega na wana ccm wenzangu tangu hatua za awali kwenye matawi lakini kitu kikubwa kwa sasa inapaswa kuvunja makundi yote ili tuungane kwa pamoja katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na nia yetu ni kushinda mitaa yote,”alisema Jungulu.

Aidha Mwenyekiti huyo hakusita kuwapongeza kwa dhati viongozi wenzake pamoja na wanachama wote kwa kuanzia ngazi za mashina na matawi hata ngazi ya kata kwa kushirikiana bega kwa bega katika suala zima la kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la makazi kwa ajili ya kupiga kura.

Katika hatua nyingine alibainisha kwamba yeye kama Mwenyekiti wa CCM Kata ya Picha ya ndege ataendelea kukijenga na kukiimarisha chama ikiwa pamoja na anashinda kwa kishindo katika mitaa yote katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Nao baadhi ya wana chama wa CCM Kata ya picha ya ndege walimshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wao kwa kujitahidi kwa hali na mali katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa wingi katika daftari la makazi kwa ajili ya kupiga kura.



Related Posts