SERIKALI INAWAJIBU WA KULINDA RASILIMALI ZA ASILI : DKT. MASANJA

Serikali ina wajibu wa kutunga sheria zinazolenga kulinda rasilimali za asili ikiwemo; misitu,wanyamapori.ardhi, na vyanzo vya maji dhidi ya uharibifu, unaofanywa na shughuli za kibinadamu ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinatumika kwa manufaa ya taifa nzima.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Dkt.Thomas Masanja wakati akifungua Kikao kazi cha Kupitia,kutoa maoni na mapendekezo kuhusu sheria zinazohusiana na maeneo ya uhifadhi Oktoba 28,2024 Jijini Arusha.
Mhe.Dkt Masanja amesema kuwa Serikali na Bunge imetimiza wajibu wake wa kutunga sheria za uhifadhi kwa kuhakikisha kuwa maliasili,mazingira na urithi wa kiasili wa nchi unalindwa na kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
“Sheria hizi zinapaswa kuweka msingi wa uhifadhi endelevu na kusimamia matumizi bora ya rasilimali za taifa”amesema Mhe.Dkt.Masanja

Aidha,Mhe.Dkt Masanja aliongeza kuwa THBUB imefanya mapitio ya Sheria mbalimbali za uhifadhi ikiwemo Sheria ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro Sura ya 284,Sheria ya Hifadhi ya Wanyama Pori Sura ya 283,Sheria ya Hifadhi za Taifa Sura ya 282,na Sheria ya Misitu ya 323, nchini na kuwa na maoni ambayo inaona vema kabla ya kuyawasilisha Serikalini ,ni vema kukaa na wadau wa sekta husika ili kupata maoni yao.

“THBUB inawajibu wa kutoa mapendekezo kwa serikali na Taasisi zake kuhusu marekebisho ya sheria au sera zinazokinzana na haki za binadamu,ili kuhakikisha kuwa sheria hizi za nchi zinaendana na viwango vya haki za binadamu vya Kitaifa na Kimataifa”amesema

Mhe.Dkt.Masanja
Pia Mhe.Dkt Masanja ametoa wito kwa washiriki hao wa kikao hicho kutoa michango yao kwa ukamilifu ambayo pia itasaida wakati THBUB inatoa ushauri kwa serikali.
“Niwaombe kufuatilia kwa umakini wasilisho kutoka kwa wataalam wetu,na kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia THBUB kushauri Serikali”amesema Mhe.Dkt Masanja


Awali Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kufanya mapitio ya sheria mbalimbali zinazohusu Hifadhi za Wanyamapori na Hifadhi za Misutu na kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho ili kupunguza migogoro iliyopo baina ya wananchi na Watendaji katika maeneo ya hifadhi.

Bw.Ntwina amesisitiza kuwa pamoja na lengo zuri la kuwepo kwa sheria za hifadhi za maeneo husika kwa ajili ya kulinda maeneo hayo, kumekuwepo malalamiko ya matukio ya ukiukwaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali hususan wakati wa ukamataji wa watuhumiwa na wakati wa kushikilia vielelezo kesi zinapokuwa zikiendelea mahakamani; pia kumekuwepo malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu za minada ya mifugo inayofanywa hifadhini wakati wa kukaza hukumu za Mahakama pamoja na malalamiko ya urejeshwaji wa mifugo pungufu baada ya kesi kumalizika Mahakamani.Hali hii imesababisha Wananchi kukosa amani na wengine kufilisika na kuleta hasara kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla.

“Mengi ya malalamiko hayo yameripotiwa katika kipindi cha takribani miaka nane sasa (8) kwa maana ya kati ya Mwaka 2016 hadi 2023 na katika kipindi hicho yamehusisha Mapori ya akiba ya Wanyama na Misitu nchini’’amesema Bw.Ntiwna.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw.Cylius Mlekwa amesema kuwa kikao kazi hiko kina tija kubwa katika kuimarisha na kuboresha mahusiano ya Uhifadhi na Wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi zote za Taifa na hifadhi ya Ngorongoro.

Bw.Mlekwa ametaja migogoro hiyo ni Wafugaji kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kwaajili ya michungo yenye rutuba ndani ya hifadhi.

“Kupitia kikao hiki namini suluhu itapatikana ya namna bora ya kuhifadhi na na kuleta tija ya watu”amesema Bw.Mlekwa.

Related Posts