Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte, amewaambia waandishi wa habari mjini Brussels nchini Ubelgiji kwamba leo anaweza kuthibitisha kuwa vikosi vya Korea Kaskazini vimepelekwa katika eneo la Kursk.
Rutte amesema mwingilio huo wa Korea Kaskazini, unaashiria kutanuka kwa vita hivyo vya Urusi nchini Ukraine.
Ukraine yasema wanajeshi wa Korea Kaskazini kuingia vitani wikiendi hii
Rutte amesema hayo baada ya ujumbe wa ngazi za juu wa Korea Kusini uliowajumuisha maafisa wakuu wa kijasusi na kijeshi pamoja na wanadiplomasia wakuu, kuwahutubia mabalozi 32 wa mataifa wanachama wa muungano huo wa kijeshi wa NATO katika makao yake makuu.
Mashauriano yanaendelea kuhusu hatua ya kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi
Rutte pia amesema kuwa NATO inafanya mashauriano kabambe kuhusu kinachoendelea ndani ya jumuiya hiyo, Ukraine pamoja na washirika wao katika eneo la India na Pasifiki.
Katibu huyo mkuu amesema hivi karibuni, anaratajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Korea Kusini na waziri wa ulinzi waUkraine. Pia ameongeza kuwa wataendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu ijapokuwa hakuruhusu maswali baada ya taarifa hiyo.
Rutte ameongeza kusema kuwa tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, zaidi ya wanajeshi 600,000 wa Urusi wameuawa ama kujeruhiwa.
Wanajeshi wa Pyongyang kupelekwa katika mstari wa mbele wa vita Ukraine mapema kuliko inavyaotarajiwa
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, amesema leo kuwa kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine huenda kukafanyika haraka kuliko inavyotarajiwa. Haya ni kulingana na shirika la habari la Yonhap.
Yoon amesema hayo katika mazungumzo kwa njia ya simu yaliofanyika kwa ombi la Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen kuelezea habari kuhusu uwepo wa vikosi vya Korea Kaskazini nchini Urusi.
Korea Kusini yadai Korea Kaskazini inapeleka askari wake kwa Urusi
Maafisa wa mataifa ya Magharibi, wamesema kuongezwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini kwa mzozo mkubwa wa Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, kunaongeza shinikizo dhidi ya jeshi la Ukraine ambalo tayari limechoka.
Mbali na hayo, takriban watu wawili wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulizi la Urusi dhidi ya mji wa Kherson kusini mwaUkraine.Haya yamesemwa leo na gavana wa eneo hilo, Oleksandr Prokudin.
Picha zilizochapishwa kwenye mtandao wa Telegram wa Prokudin, zimeonesha nyumba zilizoteketea katika jengo la ghorofa nyingi.