Israel yapiga marufuku UN kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina

 

BUNGE la Israel limepiga kura kupitisha sheria ya kupiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA).

Sheria hiyo inaondoa kinga ya kisheria kwa wafanyakazi wa UNRWA ndani ya Israel, na makao makuu ya shirika hilo yaliyopo Jerusalem Mashariki yatafungwa.

Aidha, sheria hiyo inayolizuia shirika hilo kufanya kazi ndani ya Israel na Jerusalem Mashariki inayokaliwa na Israel, ndani ya miezi mitatu.

Mawasiliano kati ya wafanyakazi wa UNRWA na maofisa wa Israel pia yatapigwa marufuku, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa shirika hilo kufanya kazi Gaza na Ukingo wa Magharibi, unaokaliwa na Israel.

Ushirikiano na jeshi la Israel, ambalo linadhibiti vivuko vyote vya Gaza ni muhimu kwa UNRWA kuhamishia misaada katika eneo lenye vita. Ni shirika kuu la Umoja wa Mataifa linalofanya kazi huko.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kutekeleza sheria hiyo, kutakuwa na madhara kwa utatuzi wa mzozo wa Israel na Palestina na kwa amani na usalama katika eneo hilo kwa ujumla.

Mkuuu wa UNRWA, Philippe Lazzarini, ameonya kuwa hatua hiyo itazidisha mateso kwa Wapalestina.

Nchi kadhaa, zikiwemo Marekani, Uingereza na Ujerumani, zimeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, amesema hatua hiyo ya Israel ni makosa makubwa, wakati Waziri Mkuu, Sir Keir Starmer, akisema sheria zinakwamisha kazi muhimu ya UNRWA kwa Wapalestina isiwezekane na kuhatarisha mwitikio mzima wa kibinadamu wa kimataifa katika eneo la Gaza.

About The Author

Related Posts