KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AJIRIDHISHA UMAIRIKAJI HUDUMA YA MAJI DAR

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefanya ziara ya kushtukiza katika makazi ya wananchi kwa lengo la kukagua upatikanaji wa huduma ya Maji Mkoani Dar es Salaam na kubaini uimarikaji wa huduma katika maeneo mengi na kusisitiza uwajibikaji wa Watumishi sekta ya maji ili kuongeza tija na huduma bora.

Mhandisi Mwajuma Waziri ameeleza kuwa jitahada mbalimbali kurudisha huduma za Maji kufuatia maboresho ya mfumo wa umeme katika Mtambo wa Maji Ruvu Juu iliyopelekea maeneo ya Kwembe, Msakuzi, Mbezi, Kimara, Kinyerezi, Bonyokwa na Tabata waliokuwa waathirika maboresho hayo.

“Nimetembelea Wilaya ya Ubungo katika maeneo ya Kimara Suka hadi Mbezi kwa Yusush na tumeshuhudia huduma ya maji kwa kiwango kizuri na maeneo mengine inazidi kuimarika, DAWASA wataendelea kufuatilia maeneo ambayo hayapati huduma kwa kushirikiana na Wananchi kupitia taarifa zitakazopokelewa kupitia vyanzo mbalimbali vya habaei” alisema Mhandisi Mwajuma

“Kimsingi hili ni agizo la Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso la kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kila eneo la kihuduma DAWASA, na iwapo kutakuwa na changamoto ya huduma Wateja wajulishwe na kuwa na taarifa” alisema Mhandisi Mwajuma.

Katibu Mkuu ameongozana na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Maji pamoja Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Mkama Bwire pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka.

Related Posts