Na. Mwandishi wetu – Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, amewataka Madereva kuzingatia tija na ufanisi katika utendaji kazi wao ili kuhakikisha jamii inafanya kazi za kiuchumi kwa usalama na muda muafaka, hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amebainisha hayo wakati wa kufungua Mafunzo ya Tija na Ufanisi wa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.
“Nchi yetu inakabiliwa na changamoto za ajali barabarani ambazo zinaathiri nguvu kazi ya Taifa na kupunguza pato, hivyo basi ni muhimu kuzingatia mafunzo haya ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika” amesema.
Akizungumza Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi, amesema lengo la Mafunzo hayo ni kutoa ujuzi na mbinu za udereva bora ili kupunguza ajali barabarani na kutii sheria bila shuruti.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, akifungua Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Ofisi hiyo, pamoja na Madereva walio hudhuria Mafunzo ya Ustadi wa Kuboresha Tija na Ufanisi kwa Madereva, leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam.