Rais Dkt. Samia afungua mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary Jijini Dar es Salaam

RAIS Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika kabla ya kufungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024. Mkutano huo unahudhuriwa na watu kutoka nchi mbalimbali, ambapo miongoni mwao ni Wenza wa Wakuu wa Nchi 15 za Afrika na Asia, Watunga Sera, Wanataaluma, Watafiti na Wanahabari wa masuala ya Afya kutoka nchi mbalimbali duniani.

Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024. Mkutano huo ni Kongamano la kielimu linalofanyika kila mwaka ili kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Bara la Afrika na Asia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024. Aidha, Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa Wenza hao viongozi kutumia ushawishi walionao kuunga mkono ajenda ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia katika nchi zao.

Related Posts