RC Kagera awapongeza wazawa wanaowekeza kwao walipozaliwa

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma Mwassa amewapongeza wawekezaji hususani wazawa wa Mkoa wa Kagera ambao wamekumbuka kwao na kuamua kuwekeza ili kuzidi kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Ameyasema hayo wakati qa uzinduzi wa awali wa ukumbi wa kisasa wa RIO DE JANEIRO uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera chini ya wawekezaji Mganyizi Zachwa na Regina Mganyizi Zachwa ambao utaongeza chachu ya burudani kwa wakazi wa maeneo hayo na maeneo jirani ikiwa ni sambamba na kukuza uchumi.

Hajath Mwassa amesema kuwa uwekezaji huo ni matokeo mazuri ya tamasha la Ijuka Omuka Festival alilolifanya Mkoani humo mwishoni mwa mwaka jana 2023,huku akiwataka wanakagera wengine kuwaunga mkono wawekezaji ambao tayari wamejitoa kuwekeza ili Mkoa uzidi kusonga mbele.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rio de Janeiro Muganyizi Zachwa amesema kuwa wamejipanga kufanya makubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera na kuweka wazi kuwa ufunguzi rasmi itakuwa ni tarehe 2/11/2024 ambapo Marioo atakuwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kutoa Burudani.

 

 

Related Posts