Kanisa liwaondoe mapadri wa kashfa za unyanyasaji – DW – 30.10.2024

Ripoti hiyo ya kina kutoka kwa Tume ya Kipapa ya ulinzi wa watoto ni ya kwanza tangu ilipoundwa naPapa Francismnamo mwaka 2014 kujaribu kushughulikia unyanyasaji ulioenea ndani ya Kanisa Katoliki. Ripoti hiyo yenye kurasa 50 ililenga kubainisha mapungufu na kukuza sera madhubuti katika Kanisa ili kulinda watoto na watu wazima walio hatarini.

Mkuu wa Tume hiyo Kadinali Sean O’Malley, amewaeleza waandishi wa habari kwamba kanisa linanyanyuka kutoka katika “kipindi cha giza” ambapo “viongozi walishindwa kwa huzuni kuwalinda kondoo wake.”

“Kwa wahanga na manusura wote, nataka niwahakikishie kuwa nia yetu ni kufanya kila tuwezalo ili kuendelea kuwakaribisha na kuwashughulikia dhidi ya mateso yote ambayo mmeyastahimili. Maumivu na majeraha yenu yametufungua macho na kuona kwamba kama kanisa tumeshindwa kuwalinda waathirika na hatukuwakutetea na tulishindwa kuwaelewa pale mlipotuhitaji zaidi. Hakuna tutakachofanya kitakachotosha kurekebisha kikamilifu kile kilichotokea.”

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis Picha: Evandro Inetti/Zuma/picture alliance

Akikiri wazi kwamba kuleta mabadiliko ndani ya taasisi hiyo ni kama “kupanda mlima”, Kadinali Sean amesema hata hivyo tayari kanisa katoliki limo katika kipindi cha mpito “ambapo uwajibikaji na kujali waathirika kumeanza kutoa mwangaza.”

Soma kwa kina: Kumekuwepo na ongezeko la taarifa kama hizi zinazotolewa na wahanga wa udhalimu wa kingono kutoka maeneo mbalimbali

Kashfa za unyanyasaji kingono zimelitikisa kanisa katoliki kote ulimwenguni na tume hiyo iliyodumu kwa muongo mmoja, pia nayo imekabiliwa na ukosoaji juu ya jukumu lake na uongozi huku wanachama wake kadha wa ngazi ya juu wakijiondoa na kutaja changamoto.

Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo Juan Carlos Cruz ambaye ni manusura wa unyanyasaji, alisema kuwa “wahanga wengi walijiua kwasababu walikosa matumaini” na kuongeza kuwa ripoti hiyo ni muhimu sana kwa kujumuisha maneno ambayo zamani yalikuwa kama mwiiko ya “imani, haki na fidia”.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa maendeleo katika kulinda watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu yalitofautiana sana duniani kote. Katika baadhi ya kanda, unyanyasaji wa makasisi bado haukuwa “suala lililotangazwa wazi”, wakati rasilimali “zilikuwa hazitoshi” katika sehemu za Amerika ya Kati na Kusini, Afrika na Asia. Imetaja mfano wa Papua New Guinea ambako vifaa vya matibabu ili kuthibitisha vitendo vya ubakaji ni ghali sana.

Soma pia: Papa Francis akemea kashfa ya unyanyasaji wa kingono Ureno

Miongoni mwa mapendekezo yake, ni kwa wahanga kupata taarifa zaidi kuzuia “michakato isiyo ya wazi ya kisheria. Imesema inahuzunisha zaidi kwa wahanga kusimulia madhila waliyopitia mara chungu nzima na kuona kwamba hakuna hatua zinazochukuliwa.

Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo Juan Carlos Cruz
Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo Juan Carlos CruzPicha: picture-alliance/AP Photo/Y. Lee

Tume pia inataka kupunguzwa kwa urasimu na kuharakisha kesi, na ikatoa wito wa uwajibikaji zaidi kwa idara za Vatican zinazoshughulikia kesi za unyanyasaji. Zaidi ya hayo, Kanisa linahitaji kurahisisha mchakato wake wa kuwaondoa mapadre wanaotuhumiwa kufanya unyanyasaji huku ripoti ikitaja “haja ya utaratibu wa kinidhamu au wa kiutawala unaotoa njia mwafaka ya kujiuzulu au kuondolewa madarakani”.

Tangu alipochukua uongozi wa Kanisa Katoliki mwaka 2013, Papa Francis amechukua hatua tofauti za kushughulikia unyanyasaji, kuanzia kufungua nyaraka za ndani za Kanisa hadi kuwaadhibu makasisi wa ngazi za juu. Pia amefanya kuwa ni lazima kuripoti tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwa viongozi wa Kanisa.

Lakini makasisi bado hawatakiwi kuripoti unyanyasaji kwa mamlaka za serikali, isipokuwa tu pale kama sheria za nchi husika zinahitaji kufanya hivyo, huku ukweli wowote unaotolewa wakati wa kuungama ukibaki kuwa wa faragha.

“Utamaduni wa ukimya” kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unazuia kuripotiwa kwa kesi kama hizo katika baadhi ya nchi za kiafrika kama vile Cameroon na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imebainisha ripoti hiyo.Maelfu ya watoto walinyanyaswa na Kanisa Katoliki Ureno

Duniani kote, ripoti imeeleza kwamba changamoto kubwa ilikuwa ni kwa Makanisa kutanguliza maslahi ya kulinda taasisi hiyo badala ya kuwajali waathirika. Barani Ulaya, licha ya hatua zaidi za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia wa makasisi, ripoti hiyo ilitaja mchakato wa polepole wa kesi ndani ya Kanisa.

 

Related Posts