Dylan Mobetto amelamba Shavu la kujiunga na Juventus Academy

Mtoto wa Staa wakike bongo Hamisa Mobetto ambaye anaitwa Dylan Mobetto amelamba Shavu la kujiunga na Academy ya timu ya mpira ya Juventus hapa bongo akiwa kama Balozi wao ambapo @hamisamobetto amempongeza mtoto wake huyo kwa shavu hilo

Hamisa ambaye ameshare good news hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii akisema.. >> “Leo ni siku ambayo, moyo wangu umefurahi !
Hongera, @dylandeetz,
kwa kujiunga na Juventus Academy Tanzania kama balozi wao mpya!

Kukutazama ukiingia kwenye ulimwengu huu wa soka kunanijaza furaha nyingi sana.
Na ukue, ujifunze, na uangaze kama ndoto zako, bingwa wangu! Mama ndiye shabiki wako mkubwa kila wakati, ndani na nje ya uwanja.” Hamisa Mobetto

Related Posts