Mfuko wa Taifa wa Maji wajivunia mafanikio ya miaka tisa katika uwekezaji wa sh.Bilioni 450

*Yajivunia kukamilika kwa miradi 354 washukuru msukumo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

MFUKO wa Taifa wa Maji ( NWF) imesema kuwa tangu kuanzishwa mwaka 2015 imewekeza miradi 998 yanye thamani ya sh.bilioni 450.

Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2024, miradi ya maji 354 kati ya miradi 998 iliyopokea fedha kutoka Mfuko wa Taifa wa Maji imekamilisha na kunufaisha wananchi wapatao milioni 5.3.

Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Wakili Haji Nandule alipozungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam.

Amesema mafanikio hayo yemechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano kutokana serikali Kuu na msukukumo mkubwa wa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

“Mafanikio yetu nguvu kubwa ni pale tulipoona kukamilika kwa utekelezaji wa miradi ya maji 354 ambapo hayo ndio kufikiwa kwa dhamira ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa wa Maji”amesema Wakili Nandule

Amesema miradi m iliyofanikiwa ni
Mradi wa Maji Isaka Kagongwa – 6.1 B
Shinyanga,62,206
Mradi wa Maji Katoro Buselesere – 2.5 B
Geita 153,472,Mradi wa Maji Nyamtukuza – 11.1 B Geita 28,731,Mradi wa Maji Kyaka Bunazi – 6.1B, Bukoba 65,470 M,Mradi wa Maji Kemondo – 4.5 B, Bukoba Milioni 117,000,Mradi wa Maji Muze Group – 3.1B, Rukwa 36,071M
Mradi wa Maji Mbabale Mbarika – 6B ,Mwanza 14,606M,Mradi wa Maji Makongorosi – 2.88B
Mbeya M 18,000 Mradi wa Maji Matwiga 4.25B.

Miradi mingine ni
Mbeya Miloni 45,000 Mradi wa Maji Luduga Mawindi 5.4 B Mbeya 21,596 Mradi wa Maji Darakuta Magugu 3.9B,Manyara 80,000, Mradi wa Maji Komuge 1.6 B Mara 25,945 Longido Kimokouwa Namanga 6.5 B Arusha
16,300M,Mradi wa Maji Ng’apa – 2.8 B Lindi
7,753 Mradi wa Maji Isimani Kilolo – 6.7 B
Iringa ,58,000,Oldonyo Sambu – 2.1 B Arusha
29,449 ,Mradi wa Maji Kintinku Lusilile 1.7 B Singida 55,485 ,Mradi wa Kikafu-Bomang’ombe – 1.49 B Kilimanjaro
55,855 Mradi wa Maji Mkwiti 4.1 B Mtwara
26,164 Mradi wa Maji Miyuyu na Mnima 4.2B.

Alisema mafanikio mengine ni kuzinduliwa kwa Dirisha la mkopo ma kuanza kutoa mikopo hadi kufikia Julai 2024, jumla ya shilingi bilioni 5.3 zimetolewa kama mikopo kwa Mamlaka za Maji

Katika hatua nyingine Mtendaji huyo Mkuu alisema,Mfuko unajivunia mafanikio ya utunzaji wa Rasimali za maji Takribani miradi 104 ya uhifadhi na uendelezaji wa vyanzo vya maji imetekelezwa ikijumuisha uhifadhi wa vyanzo vya maji zaidi ya 92 (i.e. Chemichemi, vidakio vya maji, Maziwa, Mabwawa, Mito na Visima), Ujenzi wa bwawa moja (1) na ukarabati wa mabwawa saba (7), uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 50 pamoja na kurudisha Mito mitano (5) iliyopoteza mikondo yake.
 

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) Wakili Haji Nandule akizungumza na Wahariri Vyombi vya Habari katika Mkutano wa kueleza mafanikio kwa Mfuko huo kwa kipindi cha Miaka mitatu cha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
 

Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF)Mhandisi Abdallah  Mkufunzi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari  kuhusiana na mikakati ya Bodi katika vyanzo Fedha
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prosper Bachafwe akizungumza kuhusiana na mikakati ya kuwapatia maji wananchu kutumia mfuko huo ,jijini Dar es Salaam.
 

Baadhi wa watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) pamoja na Wahariri na waandishi wa habari wakifatilia wasilisho na Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Wakili Haji Nandule,jijini Dar es Salaam.

Related Posts