Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 01,2024 ameungana na vingozi mbalimbali pamoja na mamia ya wakazi wa Mkoa huo kuaga mwili wa Mkuu wa zamani wa JWTZ Jenerali David Msuguri katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.
Tukio la Kuaga mwili wa Jenerali Mstaafu David Msuguri limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ambaye wakati akitoa hotuba yake amesema namna pekee ya kumuenzi Jenerali Msuguri ni kujitoa kwa nguvu zote kuilinda mama Tanzania.
Aidha viongozi mbalimbali wa mashuhuri wamejitokeza Kuaga mwili wa Jenerali Msuguri akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi Dkt Stergomena Tax.
Mwisho Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Msuguri alifariki dunia Oktoba 29,2024 Jijini mwanza alikokuwa akipatiwa matibabu, alizaliwa Januari 4, 1920 huko Butiama Mkoani Mara alitumikia nchi katika Jeshi kuanzia mwaka 1942 hadi 1988 akihitimisha uongozi wake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya 1980 na 1988.