Na Linda Akyoo-Siha
SHIRIKA la SHUJAAZ kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI) imeitaka jamii kufanya mazungumzo na vijana wa kike wa Kitanzania ili kuweza kubainisha changamoto zinazowakabili vijana hao katika ufugaji wa kuku na kutafuta suluhu za changamoto hizo.
Akizungumza wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wakati wa mafunzo yanayohusu Ufugaji Kuku bora, Msimamizi wa Mradi wa BINTI SHUJAAZ Bw.Lucky Komba ameziomba serikali za Mitaa kwa kushirikiana na maofisa mifugo wilaya,watendaji wa kata, vijiji, maofisa kilimo na ufugaji, viongozi wa kimila na viongozi wa kidini kuwaskiliza mabinti wafugaji.
Amesema watakapowasikiliza mabinti hao watabaini changamoto wanazopitia na kuweza kujuwa nikwa namna gani wanaweza kuwakomboa vijana wa kike wa Kitanzania wanaofuga kuku.
Hata hivyo Komba amesema kuwa shirika la Kimataifa la Utafiti wa mifugo limeona kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa vijana wa kike kuhusu ufugaji bora wa kuku.